Na Baba Juti
#WatuWaMungu mambo mengi sasa yanaanza kufichuka kuhusiana na sakata la Talaka ya JANET JACKSON na aliyekuwa Mumewe WISSAM AL MANA ikiwa ni baada ya Tukio la Kulia Stejini katika Tour yake ya A State Of World.
Safari hii Kaka yake na Janet Jackson anayeitwa RANDY JACKSON ameibu tatizo lingine ambalo lilionekana kumkwaza na hata kumuumiza zaidi Janet Jackson wakati akiwa katika Ndoa yake huko Quatar.
Randy Jackson anadai kuwa, Wissam licha ya kumfanyia unyanyasaji ambao wengi tumeusikia kutoka kwa watu wengi na vyombo vya habari vingi, bado alikuwa akimdhalilisha na hata kumfanya aione dunia chungu kipindi Janet Jackson ana ujauzito wa mtoto wao EISSA.
Kaka huyo wa Janet ambaye ni mtu wa karibu sana kwa Bibie huyo anadai kuwa, Wissam alifikia mpaka hatua ya Kumuita Mara kwa Mara Janet kuwa ni KAHABA, kitu ambacho hakikuwa sahihi kwa Dada yake.
TUNAMNUKUU
"Ilikuwa ni Hali ya Dharau kwa asilimia Fulani. Na hii ilitokea katika Mahusiano yao hapo Baadaye kabisa. Udhalilishaji wa Maneno, kufanywa Mfungwa ndani ya nyumba yake. Hakuna mwanamke mjamzito anayependa kuitwa KAHABA kila siku. Kulikuwa na Vitu kama Hivyo. na hayo ndiyo aliyopitia. Kile Mlichokishuhudia HUSTON, ni hali yake ambayo ilikuwa inajitokeza, na hicho ndicho alichopitia. Unyanyasaji bado unaendelea ni kweli wana makubaliano kimalezi, na alimruhusu aambatane na mtoto wao kwenye tour yake, lakini bado kuna uonevu. Hii Tour isingefanyika, lakini kwa Neema ya Mungu, tuko hapa na tunasali sana"
EmoticonEmoticon