Na Baba Juti
WASANII Wa Muziki wa aina tofauti kutoka Jijini Arusha, wamekutana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha , Mheshimiwa Mrisho Gambo kuzungumza masuala yao ya Muziki na kuhamasisha Utalii.
Kupitia account ya Instagram ya Mkuu wa Mkoa Huyo, Mhe. Gambo alifafanua kuwa kwa alikutana na Wasanii hao akiwemo DOMO KAYA, JCB na wengine kuzungumzia namna ambavyo wanaweza kuhusisha Muziki wao wanaoufanya na Kutangaza Utalii wa Nchi ya Tanzania hasa Mbuga za Wanyama
Tukio hilo lilifanyika Jana katika Ofisi yake huku akidai kuwa, amewaambia waandae andiko Maalum na bora ambalo litaainisha namna ambavyo watautangaza utalii wa Ndani hasa ikiwemo Mbuga mbali mbali za Wanyama
Kwa Upande wake Msanii wa HIP HOP Nchini Tanzania, Domokaya, naye alisistiza kukutana kwao na Mkuu wa Mkoa huyu, huku akiwasihi wasanii pia kujikita katika Sekta ya Utalii ili kuangalia namna ambavyo unaweza kutangazika katika mataifa mengine hasa kupitia Muziki wao
EmoticonEmoticon