REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

TCRA : KUNA WATOTO WADOGO AMBAO WANATUMIA MITANDAO YA KIJAMII (VIDEO)

1:59:00 AM
 
Na Baba Juti     
KWA mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Nchini Tanzania (TCRA) kuna baadhi ya watoto wadogo ambao wanatumia mitandao ya Kijamii ingawa Utafiti bado haujabainisha ni idadi Gan  na maeneo Gani Zaidi

Kauli hiyo imetolewa Siku ya Jana Wakati TCRA wakizindua kampeni yao mpya ya Kuwalinda na kutokomeza udhalilishaji wa Watoto wadogo kupitia Mitandao ya Kijamii, iliyopewa jina la C-SEMA

Kaimu Meneja wa Mawasiliano kwa Umma-TCRA, SEMU MWAKYANJALA amesema kuwa, TCRA kwa kushirikiana na Taasisi mbali mbali, inahakikisha kabisa Watoto wadogo hawapati madhara kutokana na huduma za mawasiliano na ndio maana walitoa namba maalumu ya CHILD HELP LINE ambayo ni 116, ili kuhakikisha kama kuna tatizo lolote kuhusu mtoto, basi taarifa itolewe ili kutoa msaada haraka

Naye THELMA DHAJE ambaye ni Meneja wa Simu ya Huduma kwa Watoto ya C-SEMA, amedai kuwa ukuaji wa Utandawazi, umesababisha pia baadhi ya watoto wadogo kutumia mitandao ya Kijamii ingawa hakuna takwimu kamili ambazo zinaonesha kuwa ni Idadi gani ya watoto ambao wanauwezo wa ku-access katika mitandao hiyo ya kijamii.

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER