Na Baba Juti
INAWEZA ikawa ni Njia moja wapo ya kuhamasisha hasa lengo kubwa ikiwa ni kwa wanawake ambao wanapatikana Barani Afrika, ukizingatia Tamaduni zetu zilivyo
Alicia Keys na Mbunifu wa Mavazi kutoka uingereza, Stella McCartney, wameamua kuvalia njuga suala la Kansa ya Titi kwa Wanawake Wengi ambao ni waafrika lakini wanaishi Nchini Marekani
Alicia ambaye pia anadai kuwa mama yake ni mmoja kati ya Watu walioponea chupu chupu katika Tatizo la Ugonjwa huo wa Kansa ya Titi, amesema kuwa kuwa kwa mujibu wa Takwimu ambazo zipo wazi, ni kwamba wanawake wengi ambao ni African-American kwa asilimia 45, hubainika kuwa na kansa ya titi iliyokomaa kuliko wamarekani weupe kwa sababu hawana muamko wa kupima na kubaini matatizo yao
Ukiachilia mbali suala la kupima, pia hata Nguo za ndani wanazovaa, yaani Braa, huchangia kwa asilimia kubwa kupatikana kwa Tatizo hilo
Mbunifu wa Mavazi Stella, pia amethibitisha kuwa alimpoteza mama yake kwa tatizo hilo hilo, hivyo ameamua kufanya kazi na Alicia keys, ikiwemo kubuni Bra ambazo zitasaidia kwa asilimia kubwa kupunguza maambukizi yasiyo naulazima
EmoticonEmoticon