KENYA
#WatuWaMungu Msanii SWABRI MOHAMED maarufu kama REDSAN ameamua kuuvunja ukimya kuhusu hatua ya Waandaaji wa Matamasha Nchini Kenya kutokumhusisha ama kutokumpa chance katika Matamasha yao
Redsan ambaye amekuwa katika Soko la Muziki wa Kizazi Kipya Afrika Mashariki kwa Takriban Miaka 15, amedai kuwa ni kweli kuna baadhi ya Wasanii wenzake Nchini Kenya ambao hufanya Shows mara kwa mara Ndani ya Kenya, lakini yeye imekuwa ni Ngumu kwa sababu ya gharama ambazo anatakiwa Kulipwa.
Hitmaker huyo wa BADDER THAN MOST ameongeza kuwa, waandaaji wengi wamekuwa wakishindwa kumpata kwa sababu ya Masharti magumu hasa katika Malipo kutokana na mkataba wake na RECORD LABEL yake ya Kimataifa ya SONY GLOBAL
Record Label yake hiyo imekuwa ikitoza Gharama Nyingi sana kwa wanaohitaji Show na yeye, na hiyo ni kutokana na namna ambavyo wanawekeza katika Muziki wake
TUNAMNUKUU
"Unajua, Vitu vingi sana vimebadilika tangu miaka kdhaa iliyopita. Moja ni kwamba nimesaini mkataba na SONY GLOBAL ambao wananimanage kwa hivi sasa. Ukinipigia kwa ajili ya show hivi sasa, makubaliano ya mkwanja na Management yangu yako juu kwa sababu wamewekeza sana katika muziki wangu na mie mwenyewe na Mapromota wengi wa Kenya hawajawahi kukutana na mahitaji haya. Mapromota wanaweza kuwekeza sana kwa wasanii wa nje hata kama wasanii wazawa wahapa tunazalisha muziki wa Ubora ule ule. Ni kwa sababu hii kuwa napata show chache hapa nyumbani, lakini nje ninapata Nyingi sana sababu wanaweza kukidhi hali yangu kimasoko."
EmoticonEmoticon