REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MWANZA !!!: KUNGUNI WANAVYOWATESA ABIRIA KATIKA DALADALA

5:39:00 AM

Na Sadick  Mwenda  
#WatuWaMungu kuna taarifa ambazo Baba Juti Blog tumezipata na tukaona sio mbaya kushare na Nyie, hakuna mtu ambaye hawafahamu Kunguni

Kwa Mujibu wa Wakazi wa Mwanza wanaotumia Usafiri wa Magari madogo ya Umma maarufu kama "Dala Dala" katika Jiji la Mwanza, wamedai kuwa kuna tatizo la Kunguni katika Magari hayo, kitu ambacho kimeonekana kuwapa hofu watumiaji wengi wa Usafiri huo

Wakizungumza na babajuti.blogspot.com leo asubuhi katika Kituo cha Magari kilichopo Soko Kuu, Wakazi hao wamelalamika kukutana na adha hiyo katika daladala mbali mbali mbazo wamekuwa wakipanda

Akizungumza kwa Hizia kubwa kuhusu hilo, Mkazi wa Eneo la Bwiru amedai kuwa ameshakutana na Kunguni hao si zaidi ya Mara moja, hali ambayo imesababisha kuwahamishia nyumbani kwake.

"Yaani Mara ya kwanza nilidhani mie ndio ninao, nikaona aibu kusema maana wale wadudu sio wa kawaida. cha ajabu, leo wakati nimepanda gari ya Bwiru - Kisesa, nikaona kwenye Siti ya Mbele, kuna kunguni kama wawili wakaongozana. Ikabidi nipekue, kutizama hivi, nikaona balaa la Kunguni na Mayai yake" alisema Bi. Bhoke Mutaira


Tofauti na shuhuda huyo wa Kwanza, Mwingine alidai kuwa ameshakutana nao sio jana wala leo, ila ni muda Mrefu, kitu ambacho kinampatia umakini mkubwa sana katika Usafi
"Kunguni hawa wapo muda tu, hasa kwenye mafgari yenye Siti chafu kabisa. si unajua hawa wakiamka, wao wanajali abiria tu, na sio usafi. mie nimeshawabeba mara nyingi mno, na mpaka sasa niko makini. hasa hizi gari za Kisesa kuja Mjini au Machinjioni kuja mjini na hata Bugarika kuja Mjini, yaani ndo zimejaza hawa wadudu" alisema Boaz Marundi

Walipotafutwa Madereva na Makondakta kujibu suala hilo, nao hawakusita kuzungumza
"Kwenye Gari langu hawamo maana ninazingatia usafi, lakini nimesikia pia kwenye Magari mengine wapo. hii ni kwa sababu tunakutana na abiria mbali mbali, na huwezi kusema unamkagua kama ana kunguni au lah. ila asilimia kubwa, Abiria wenyewe Ndio wanaowaleta" alisema mmoja wa Madereva katika Stand Hiyo ya Magari yaendayo Bieru

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER