Na Baba Juti
#WatuWaMungu Mnamkumbuka KEISHA CORE?, yule Bibie aliyeusumbua Ulimwengu na Mkwaju wa Dunia unaoitwa SENT FROM HEAVEN
Sasa huenda akalipa mabilioni Ya Fedha baada ya kushtakiwa na Mchepuko wa Birdman... Upo hapo?
kama utakuwa na kumbu kumbu Nzuri, Mwaka 2014, Birdman alikuwa "akimtindua" Keisha Core na kila kitu kilikuwa wazi kabisa, lakini baadaye mambo yakawa tofauti kabisa kabisa baada y uhusiano wao kuishia pabaya
Kwa Taarifa ambazo tuliwahi kuzimimina kupitia Hit Zone, ni kwamba Keisha Core alikuja kumfumania Birdman na Mwanamke huyo ambaye alikuwa ni Msaidizi wa Ndani, ambapo Keisha alimkuta Binti huyo kajificha Bafuni ili kuepuka Mfumanio mzito lakini ikabumbuluka
Baada ya Fumanizi hilo, Keisha Core alimuonesha Ubabe Binti huyo hasa kwa Kipigo, ikiwa kama ni adhabu ambayo unaipata ukifumwa tu unakunjuka na Mume wa Mtu.
Sasa Habari Mupya ni kuwa Bibie huyo anahitaji Keisha Core amlipe USD Milioni 4 sawa na Tsh 9,124,000,000 kutokana na kitendo alichomfanyia.
Sasa unaweza kujiuliza kuwa ni kwanini anahitaji mkwanja huo Mrefu, Bibie Huyo kaugawa kama ifuatavyo
- USD 500,000 Kwa ajili ya Matatizo hasa Kihisia
- USD Milioni 2 Kwa ajili moja kati ya Kiungo cha mwili kudhurika na hata kutokufanya kazi kabisa
- USD Milioni 1.5 kwa ajili ya Maumivu aliyomsababishia
- USD 200,000 kwa ajili ya Matibabu mengine yajayo ambayo anatakiwa kuyapata
- USD 50,000 kwa ajili ya kipato alichopoteza kutokana na kuuguza majeraha na muda aliopoteza wote
- USD 300,000 kwa ajili ya kipato chake ambacho angepata muda ujao kama angekuwa kazini
Sasa Hata Hivyo, SABRINA ambaye ndiye muathirika, amedai mahusiano yake na Birdman hawezi kuyazungumzia maana hakuna ukweli wowote wa kile ambacho kilitajwa kama sababu ya Keisha Core kumpa Kipigo
EmoticonEmoticon