Na Baba Juti.
#WatuWaMungu Siku Ya Jana , Jamii ya Hip Hop ilikumbwa na Majonzi Mazito baada ya kumpoteza mmoja kati ya Members ambao wanaunda kundi la Mob Deep ALBERT JOHNSPN a.k.a PRODIGY
Taarifa ambazo Team Hit Zone tulizipata Siku ya Jana, zinadai kuwa Rapper huyo ambaye amefariki akiwa na Umri wa Miaka 42, alikutwa akiwa amefariki Nyumbani kwake huku sababu ama chanzo kikiwa hakijabainika mpaka Hivi sasa
Lakini kwa Taarifa ambazo tuko nazo mpaka Hivi sasa, ni kwamba Prodigy alikuwa akisumbuliwa na Tatizo la Sickle Cell Anemia siku chache Zilizopita, na kulazwa Hospital baada ya Perfomance yake huko LAS VEGAS, Marekani
Tatizo hilo limekuwa Likimsumbua tangu amezaliwa, na amekuwa akifanya Juu Chini ili kusurvive katika Maisha Yake ya Kila Siku
50 CENTS: PRODIGY ALINILINDA SANA !
Mwaka 2005, Mobb Deep walisain Mkataba na G UNIT na kuanza kufanya Kazi pamoja. Mkwaju wa OUTTA CONTROL (Remix) wakiwa na 50 Cents ndio uliowafanya wathibitishe Uwezo wao
Siku Hiyo hiyo ya Jana, 50 Cents alilazimika kuondoka katika Tuzo za GOLDEN NYMPH (Golden Nymph Academy Awards 57) baada ya kupata Taarifa Hizo, huku akiandika Mengi kuhusu Yeye.
Katika Hatua ya Kwanza, 50 Cents aliandika Hivi:
"Police walijitahidi kumtumia P ili wanikamate. Walimuuliza kama nilikuwa ninamiliki silaha ama Dawa za Kulevya. Kisha walimuamuru aweke Bunduki katika Gari langu . hakufanya Hivyo, na badala yake aliniambia kila kitu ambacho walikuwa wanajaribu kufanya."
katika hatua Nyingine, Hit Maker huyo wa In Da Club aliandika hivi
"Pumzika kwa amani Prodigy, utapendwa na kukumbukwa Milele. Mungu akubariki na Familia yako. Nimekosa maneno ya kuzungumza. ilinilazimu kuondoka katika sherehe za Tuzo"
EmoticonEmoticon