Na Baba Juti
#WatuWaMungu Binti wa Miaka 18 amehukumiwa Kifungo cha Miaka 20 Jela baada ya Mahaklama kubaini na kuthibitisha kuwa alihusika katika Wizi na kumpiga Risasi Kijana Mwenzake Kupitia App ya Mahusiano ya Kimapenzi.
Hakimu MATTHEW FOXMAN kutoka CENTRAL CALIFONIA, alitoa Hukumu Hiyo kwa Mshtakiwa huyo anayetambulika kwa jina la KY'ANDREA COOK, na kuiacha Familia yake akiwemo mama yake Mzazi ikilia na kuhuzunika kwa Uchungu
Taarifa kamili zilifafanuliwa Kuwa, Mnamo mwezi March mwaka 2017 Ky'andrea akiwa ni Mwanafunzi wa MAINLAND HIGH SCHOOL Huko Huko Nchini Marekani, alimrubuni Kijana mwenye Miaka 27 kupitia Mtandao wa unaopatikana katika Smartphone "MEET ME " ambao ni maalum kwa Mahusiano.
Katika Makubaliano yao, Wawili hao walikubaliana kukutana katika eneo linaloitwa SOUTH DAYTON, ambapo Jamaa huyo anayetambulika kwa jina la PERRY NIDA alitarajia kumuuzia Bangi na kisha Kwenda kufanya Tendo la Ndoa kama ambavyo walipanga.
Lakini kama unavyojua Michezi hii ya Sikufahamu , hunifahamu, Jombaa Nida aliamua kumtanguliza Kijana wa Miaka 17 anayeitwa IMANNUEL PURSEL kama "Chambo", na Ndipo Chambo huyo alipopigwa Risasi na Boyfriend wa Mshtakiwa ambaye alikuwa akisubiri kuwaibia kama ambavyo walikuwa wamekubaliana na Mshtakiwa
Mama Mzazi wa Mshtakiwa alimwaga Kilio Mahakamani wakati Binti yake anapelekwa Rasmi Gerezani.
Kijana aliyepigwa Risasi Hali yakle inaendelea Vizuri sasa Hivi....
EmoticonEmoticon