Na Baba Juti:
#WatuWaMungu tunaamini kabisa katika Records Labels ambazo
zilisumbua Sana sana kipindi Cha Nyuma, kwenye Tano Bora, isngeacha Kuitaja
MURDER INC ambayo ilikuwa na Wasanii wakali JA RU:LE pamoja na ASHANTI
.
Lakini Baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Murefu huku wasanii
wakifanya Shughuli zao Nyingine, hatimaye tamko Rasmi Limetolewa kuhusu Ujio
Mpya wa MURDER INC
IRV GOTTI ambaye ndiye Mmiliki wa Record Label hiyo Kupitia
Instagram aliandika Kuwa, MURDER INC Itazinduliwa Upya na Kuanza Kupiga Kazi
upya kwa Nguvu zote, hivyo wadau wa Kazi zao wakae tayari kwa ujio huo ambao
hautowafanya walaumu kilichofanyika
Lakini Ndugu zangu, kama Mlikuwa mnatarajia kusikia kuwa
Ashanti na Ja Rule watakuwepo kuamsha kunako MURDER INC, kitulizeni kwanza ,
kwa sababu GOTTI anakuja na wasanii wengine kabisaa, ambao ni Wapya
Tunamnukuu:
“ Niko Mbioni kuzindua Tena MURDER INC RECORDS. Nina wasanii
wapya, na Muziki Mpya. Harakati ni Zile Zile, na Hii Ndiyo Record Labe yenye
Kipaji Duniani kote. Kila Mtu alifurahia sana kipindi Cha Nyuma. Nilikuwa
nikimsaidia kila mtu aliyenijia na kulia Shida zake. Nilikuwa nikipanga na
kujikuta napoteza vitu vingi ilimradi kila mmoja apate chakula. Nilimpongeza
kila mtu aliyestahili. Wala siku hata na Mfupa wa Chuki ndani ya Mwili wangu. Napenda kuwaona
Marafiki zangu wanashinda na kula vizuri. Lakini sasa hivi, ni zamu yangu sasa.
Pesa yangu ni haki yangu”
EmoticonEmoticon