DJ SNAKE |
Na Baba Juti
Sasa, hii System inaelekea kuwa Ya Moto zaidi kiasi kwamba
watu inabidi muwe makini zaidi aisee.
Mwaka 2014, DJ SNAKE na LIL JOHN walishtua Ulimwengu wa
Burudani na kuwafanya Baadhi kuwa Wehu hasa unapopigwa Mkwaju wa TURN DOWN FOR
WHAT, lakini kumbe Mzigo huo ulikuwa ni Wa Kuiba mazee
LIL JON |
Kampuni ya GOLDEN CROWN PUBLISHING ndio ambao wamefungua
Mashtaka hayo siku ya jana, dhidi ya Wasanii hao wawili, wakidai kuwa Rapper
FREDDIE GZ ndiye mmiliki halali wa Idea na Mkwaju huo wa Turn Down For What,
na yeye ndiye alikuwa Msanii wa Kwanza kuuachia.
Kampuni hiyo ambayo inawakilishwa na RICHARD BUSCH ambaye
pia laikuwa katika Upande wa Utetezi katika Wimbo wa “Blurred Lines” na
hatimaye familia ya Marvin Gaye kushinda, anadai kuwa Watu watatu ambao ni
FREDLEY SAURE (Freddy GZ) MALIKI SANKOH na ROBERSON BONJEAN, ndio waliopika
Idea ya TURN DOWN FOR WHAT mwaka 2012.
FREDDIE GZ |
Pia maelezo yanaendelea kumiminika kuwa, Mwaka 2013
walifanikiwa kurekodi mwaka 2013 na
kisha kuachiwa Rasmi March Mwaka 2013. Kitu ambacho Freddie GZ anakiongeza ni
kuwa, baada ya kuachiwa tu, basi mitandao mingi ya Kijamii na hata watangazaji
mbali mbali wa Radio za Hip Hop Nchini Marekani waliukubali na kuutabiria Mengi
Mazuri
Lakini mnamo July 2013 walioshangaa kumuona Lil Jon na Dj
Snake wakitweet kuhusu neon TURN DOWN FOR WHAT, mara LETS GO, na kisha Mkwaju
kuachiwa Rasmi
“Baada ya Freddie GZ kuachia Wimbo wake March 2013, Dj Snake
na Lil Jon waliachia tena wimbo wenye Jina Hilo hilo, na Kutumia vionjo vile
vile vya Kazi ambayo ni Original” walidai walalamikaji
EmoticonEmoticon