Na Baba Juti.
P. DIDDY kwa Mwaka huu pia alitangazwa na Forbes kuwani Msanii wa Hip anayeshikilia namba 1 kwa kumiliki mkwanja Mrefu kuliko wengine wote Dunia, kitu ambacho kimekuwa ni Muendelezo kwa Msanii huyu wa Hip Hop na Mjasiliamali pia.
Lakini Jambo ambalo Diddy amelisema ni kwamba, alichukua Uamuzi wa Kuwaandikia Barua Forbes kuwa, anawaomba wasimuandike ama kumuweka katika Orodha hiyo kwa Miaka inayoendelea kwa Sababu kuu mbili ambazo kwake ni za Msingi na hata jamii itaelewa kabisa.
Sababu yake ya kwanza ni kwamba, Forbes wanavyomuandika vile kuwa ana mkwanja wa kiasi hicho, Basi wengi huamini kuwa Rapper Huyo ana pesa hizo katiika account yake ya Bank, kitu ambacho sio Kwel;i, kweny account yake hana kiasi Hicho, ila Namba hiyo hutokana na Harakati anazofanya pamoja na makadirio ya kiasi cha fedha, ingawa ni kama Baraka kwake
Sababu Kuu ya Pili, Diddy amedai kuwa, hivi sasa hataki na hapendi kuwa maarufu kwa kuongoza kumiliki kiasi kikubwa cha fedha, bali anatamani kuwa maarufu na hata kuheshimika zaidi kwa kutoa Misaada, na anatamani akamate namba moja katika Hilo.
EmoticonEmoticon