REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

MAADHIMISHO YA SIKU YA MABOGA: IZZO BUSINES ANADAI KUWA UBACHELOR ANAOISHI DAR, UMEMFANYA ASHINDWE KULA MABOGA MPAKA ATAKAPORUDI KWA MAMA YAKE (AUDIO)

6:39:00 AM

Na Baba Juti & Cathberth Mazigo
KAMA wewe unapenda kula kula kama wengine ambao tulishajaliwa kula vyakula vya aina tofauti tofauti sana, basi utakubaliana na mie kabisa kuwa, Kuna Chakula ambacho ni Jamii ya Tunda kinachoitwa BOGA

Boga haizalishi Tunda tu, bali hata majani yake huwa ni Mboga Nzuri, na unaweza kuiita Msusa, au kuyapika Kama Mrenda kwa jamii mbali mbali kama vile wasukuma, Wanyamwezi na wengineo
Lakini Kama Haitoshi , unaweza kufurahia Juice ya Maboga, na Hata Ile Mbegu yake, hutumika kama kitoweo pia, na hunoga sana ikiwa na Viazi Vitamu

LEO, OCTOBER 26, Ni Siku Maalum ya Maboga, na huazimishwa Sehemu Mbali mbali Hapa Duniani, lakini Pia Huazimishwa kwa Njia Tofauti.

Baadhi ya Mataifa Husherekea na kutumia Maboga kama kihisishi cha Siku ya HALLOWEEN, Lakini kuna Badhi ya Mataifa hupinga Vikali matumizi hayo ya Maboga katika Siku Hiyo

Mataifa hayo huamini kabisa kuwa, Heshima ya Boga Ni Chakula Maalum na siku ya Maboga ni Siku ya kufaidi kitu Kizuri na Rahisi zaidi kupika ama kuandaa.

Tofauti na hayo, Boga kwa Kiingereza huitwa PUMPKIN , jina liliotokana na Lugha ya Kigiriki ambao huliita PEPON wakimaanisha TIKITI MAJI KUBWA

Ukiachana na Hilo, Ufaransa huliita Boga kama POMPON, Kisha Uingereza wakaliita PUMPION, lakini Wamarekani Wakaliita PUMPKIN na ndivyo linafahamika hivyo Tayari.

Izzo Business , Msanii wa Kizazi Kipya Hapa Nchini Tanzania, anasema kabisa kuwa Ni Kitu ambacho Huwa anakipenda, ila kutokana na Maisha ya Kibachelor ambayo anaishi Dar, hajala Boga Muda Mrefu wala Mboga ya Msusa, lakini akienda Mbeya kwa Mama yake, lazima alikule
Lakini Pia, anakiri kuwa anapenda sana hicho kitu na anajivunia kulipenda


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER