na Baba Juti
BARUA ambayo Marehemu Tupac aliiandika kipindi
Yuko Gerezani, inaweza kuwa ya kwako kwa Kiasi cha USD 225,000 sawa na takriban
Tsh489,375,000
Barua Hiyo iliandikwa na Pac Mwaka 1995
alipokuwa Gerezani, baada ya kupatikana na hatia ya Ubakaji, na ilikuwa inaelekea
kwa Muajiriwa DEATH ROW pamoja na
Mhariri wa jarida la DEATH ROW, NINA BHADRESHWAR.
Barua Hiyo pia, ilikuwa Na Kurasa Tano, huku
ikifafanua kuhusu Madai ya Ubakaji, yaliyompeleka Gerezani.
Tofauti na Hilo, katika barua hiyo kulikuwa na
maelezo Mbali mbali kuhusu Kijana Mmarekani Mweusi, pamoja na kuacha maisha
korofi-Yaani Thug Life
Moja kati ya aya ambazo zinapatikana katika
barua hiyo, zinasomeka hivi.
“Maisha ya Kihuni na Kikorofi (Thug Life) kwangu
hayapo Tena. Kama Yanaonekana kuwa mazuri na halisi , basi Mtu Mwingine
ayaendeleze, maana Mie Nimeyachoka tayari. Wengi hawajawahi kupona katika
Maisha ya Kihuni na Kikorofi, nabadala yake walikuwa waathirika wa Vifo. Boss
Mtafutaji wa Ukweli, anajua ni Lini anatakiwa kupiga hatua. Unatakiwa uucheze
mchezo, na Sio Mchezo ukucheze wewe. Wasio na akili, hujikita kwa wanauwake na
Ngono, lakini Kwa Wenye Akili Hujikita katika Kutafuta maisha. Bossi mtafutaji
Mfikiriaji, Kiongozi, Mjenzi, Mtengeneza pesa, Mwanajeshi, Ni mwalimu, na Zaidi
ya Yote ni MWANAUME. Ninatakla Marafiki zangu wote wafahamu kuwa, kuna hatua
Nyingine”
EmoticonEmoticon