WELCOME TO ..... (KARIBU KATIKA..)
REPIN ROCK CITY
PROJECT STUDIO: KUTANA NA HARSHBASE RECORDS WAKIZUNGUMZIA STUDIO YAO NA NAMNA WANAVYOFANYA KAZI (AUDIO)
Na Baba Juti (@babajuti)
HARAKATI za Kufahamu Recording Studios ambazo
zinapatikana Mitaa Mbali Mbali ya Jiji la Mwanza ndo Imeshaanza.
Dhumuni Kubwa ni Kuzipa nafasi Studio Hizi za
Muziki kusikika, na hata kutambulika namna ambavyo wanafanya kazi.
Hii Pia ni kutoa Fursa kwa wao kuzungumzia Ugumu
ama Changamoto wanayokutana nayo, bila kusahau undani wa Kile kinachofanyika
katika Studio Hizo.
WIKI, Nimeweza Kutembelea Studio za Harsbase
(Harshbase Records) zinazopatikana katika Mtaa wa BUZURUGA MITI MIREFU, Jijini
Mwanza.
Wasikilize hapa
INAWEZEKANA ROCK TOWN IKARUDI KWA KISHINDO BAADA YA MABORESHO HAYA?
Na Baba Juti
INAWEZEKANA Ujio wa ROCK TOWN RECORDS ukawa na
Utofauti baada ya Kukaa Kimya kwa Muda Kadhaa, ikiwemo kutokuachia Kazi Yoyote
Mpaka hivi sasa
Chanzo Cha Studio Hiyo Kukaa Kimya, ni pamoja na
Kufanya Ukarabati na maboresho kwa ajili ya Wateja watakoifika hapo kwa ajili
ya Kufanya kazi.
Tofauti na maboresho, Rock Town Records Chini Ya
Mkurugenzi Wake, Mkubwa Hermidou, Imekuja na Project ya T-Shirt ambayo ina Logo
Mpya kabisa na za kibunifu- ROCK TOWN RECORDS.
Katika Logo hiyo, Kuna Jiwe Maarufu
linatambulisha Jiji la Mwanz\a (Bismark Rock) hali inayoifanya kuwa Tofauti na
Studio Nyingi za Mwanza
HII NDIYO ZAWADI AMBAYO H BABA KAMNUNULIA MWANAE TANZANITE KATIKA BIRTHDAY YAKE
MSANII wa “Bongo-Bolingo Flava”, H BABA, amedai
kuwa amempa Zawadi ya Kiwanja, Mwanae wa Kwanza, TANZANITE ikiwa ni ndani ya Siku yake Maalum ya
Kuzaliwa, yaani Birthday.
Kupitia Ukurasa wake wa Face Book, H baba anadai
kuwa, Dhumuni la Kufanya hivyo, ni kumpongeza Mama Yake (Mke wa H baba-Flora
Mvungi) kwa Kumvumilia.
Hiki Ndicho alichoandika:
“MWANANGU @tanzanitehbaba NIMEMPA ZAWADI YA #KIWANJA
#MAENEO
YA MBEZI BEACH CHENYE UKUBWA WA #52 KWA 44 ZAWADI HII NI YA #birthday
YAKE YAKUZALIWA KWAKE NAMSHUKURU MAMA TANZANITEONE KWAKUNIVUMILIA KUPATA
MSHANGAO WA KIWANJA CHA MWANAE #HAKUTEGEMEA
#KIUKWELI
MBEZI BEACH UWANJA SIO MCHEZO KWAWANAOJUA THAMANI YA ARDHI #WANAELEWA
NINI NAMAANISHA #SIWEZI
KUMPA MWANANGU ZAWADI YA GARI KWASABABU #BADO
MDOGO PIA KIWANJA KILA ANAVYOKUWA NAKIWANJA KINAPANDA #THAMANI
ILA GARI #LINASHUKA
THAMANI #NAMSHUKURU
MWENYEZI MUNGU KWAKUFANIKISHA HILI KUBWA KWA MWANANGU @tanzanitehbaba haya haya
walee wa mbezi beach #JIRANI
YENU MPYAA”
NOT THIS TIME AGAIN… CHRIS BROWN ANAFUNGULIWA KESI TENA YA KUMPIGA MWANAMKE?
LETS hope kwamba Kila Kitu kitaenda
Fizuri kwa Baba Royalty Himsefu, Chris Brown
Mwanamke mmoja amemtaja Breezy
katika mashtaka yake, kwa Kuhusika Kumpiga na kuharibu Simu yake, baada ya
Kusukumwa kutoka kunako Bas Tour la Mkali huyo wa LOYAL
Kwa Mujibu wa maelezo ya Bibie huyo,
anadai kuwa Tukio hilo lilitokea SEPTEMBA 14, ambapo Bus Hilo la Chris Bizzo
lilipaki Nje ya Strip Club ama Club ya Akina dada wacheza Utupu, kipindi
ambacho FETTY WAP, Breezy na French Montana walikuwa wakifanya Video.
Mwanamama Huyo anaendelea Kudai
kuwa, Alijikuta akisukumwa kutoka Ndani ya Bus hilo, na Kuanguka Nje kisha Simu
yake Kuharibiwa, lakini ni baada ya Kuambiwa Kuwa haruhusiwi kuingia Ndani ya
Basi hilo na Vitu kama Kamera, ama Kitu chochote Cha Kurecord, sheria ambayo
iliwekwa na Chris na Watu wake
Jeshi la polis nchini marekani,
wanafanya uchunguzi Juu ya Tukio hilo, nab ado wanahitaji kufanya mahojiano na
Baba Royalty pamoja na watu wake
RICK ROSS AMESHINDWA KUFUA DAFU MBELE YA LMFAO
THE BIG BOSS Kutoka Ufalme wa
MMG-Rick Ross, Mwaka huu unaweza kumalizika kwa Kupigwa Chini katika Kila madai
anayofungua, huku yale anayofunguliwa dhidi yake, yakimkomba Mkwanja Mrefu.
Kama Utakuwa unafahamu tangia
Kitambo, Rozay alifungua Mashtaka dhidi Ya Kundi la Pop Nchini Marekani, LMFAO,
kwa Madai kuwa wanatumia Maneno yake, ambayo ni EVERY DAY I’M SHUFFLIN, hivyo
anawataka kuacha kutumia Swagg hiyo, maana inatokana na maneno yake ya EVERY
DAY I’M HUSTLING kunako Mkwaju wa HUSTLING
Kesi Hiyo ilifunguliwa Mwaka 2013,
ambapo Rozay alikuwa anadai kuwa, Yeye Peke yake ndo ana haki ya Kutmia kauli
Hiyo, na kitendo cha Kundi Hilo la LMFAO kufikia hatua ya kuprint mpaka T-Shirt
ya Slogan Hiyo, ni Ukiukwaji wa hakimiliki Yake.
Lakini Hakimu ambaye alikuwa anaendesha
Kesi hiyo, alimkata maini kabisa Rick Ross kwa kusema kuwa, hakuna haki Miliki
ya Neno Hustin ambalo Rozay analalamikia, hivyo Kesi hiyo haina Mashiko.
Katika Kufafanua zaidi, hakimu Huyo,
Kathleen Williams, amesema kuwa, Wimbo wa HUSTLIN alioutoa Mwaka 2006, utabaki
na Hakimiliki ya Wimbo kama Wimbo, na Sio Neno ama Kauli Mbiu.
Katika Kutoa Mifano, Judge William
alinukuu Misemo kama Vile “Holla Back”, “We Get It Poppin” na Mengineyo, kama
vitu ambavyo havina Copyright lakini Vinatumika na Kila Mtu
DULLY SYKES HATAKI U-TEAM KATIKA INSTAGRAM
Mtandao wa Instagram ni mtandao wa
kijamii ambao umetokea kuwa na mashabiki wengi sana Tanzania hivyo wengi
wanaamkia huko asubuhi mchana na mpaka usiku na kumekua na team zinatengenezwa
kwa wale wenye mapenzi na watu flani.
Dully Sykes ametangaza rasmi hataki
kutengenezewa team ya aina yoyote, anakubali mashabiki wenye upendo nae ila
hataki mtu atengeneze team manake zinamtengenezea uadui na watu wengine pale
team inapotumika vibaya.
TUNAMNUKUU
"Sitaki kuwa huko sababu
nitatengeneza maadui, hawa wanaonisuppot kila siku nitabaki nao tu ila kama
wataongezeka waongezeka kwa nguvu za Mungu na sio ushabiki wa kitimu."
"Timu za Instagram zimeharibu
hali ya hewa sasa hivi, zamani sisi kulikua kuna makundi yanashindana kwenye
bongofleva lakini sio kushindana kwa ugomvi, ni kazi inapigwa alafu baadae
tunatembeleana, na kulikua kuna Camp ikiwemo Misifas Camp ya kwangu, pamoja na
kushindana kote lakini tulikua tunakaa tunakula na kunywa pamoja”
Dully Sykes ni miongoni mwa mastaa
wa Tanzania ambao kwenye page zao za Instagram hawamfollow mtu yeyote, mwingine
kwenye hiyo list ni Ali Kiba ambapo wote wanasababu zao kwanini imekua hivyo.
JB: MAREHEMU KUAMBIANA ALIKUWA CHADEMA..SITAKI UTOTO NIKITANGAZA KAZI ZANGU…
INAWEZEKANA Mashabiki wakawa
wanakosea sana hasa pale wanapoamua kutengeneza kitu ambacho kiujumla
hakitakiwi kuwapo katika mchakato mzima wa kuhusisha Burudani, na shughuli
Nyinginezo.
Mkali kutoka Bongo Muvi, amejikuta “akijaa
Povu” baada ya Mashabiki kadhaa kumfika pabaya na kudiriki kuhusisha Kazi zake
na Suala la Siasa.
Mashabiki wa Soko la Filamu Nchini Tanzania,
wamejikuta wakishindwa kwenda sawa na Jacob Steven, ikiwa ni baada ya Big Bos
Huyo wa JERUSALEM FILM kupost Muvi Mpya ambayo Marehemu Adam Kuambiana
ameshiriki, na Filamu hiyo inaitwa MAHABUSU.
Sasa, kilichotokea ni Watu Kuanza
kumuambia kuwa, akauze Kazi Hiyo kwa Wana-ccm, ukizingatia kuwa Jb Yuko CCM.
Baada ya Kukerwa sana na hayo, JB
aliwaka na kudai kuwa, Marehemu Kuambiana alikuwa Mwanachama wa CHADEMA Kuliko
Wengi wao.
Pia ili kukazia Zaidi, JB amesema
hataki UTOTO akitangaza Kazi zake, na kama haupendi , Piga Kimya
JB aliandika Hivi
NARUDIA
TENA SIASA SIO VITA...MAREHEMU ADAM ALIKUWA CHADEMA KULIKO WENGI WENU..MPAKA
ALIKUWA CAMPAIGN MANAGER WA MKEWE JANET KULE KAWE KWENYE UDIWANI...MBONA
TULIKUWA TUNASHIRIKIANA???WASANI MBONA WENGINE WAKO UKAWA LAKINI BADO NI
MARAFIKI...NINA NDUGU AMBAO WAKO UKAWA NA NYINYI PIA MNA NDUGU WAKO CCM
MNAGOMBANA NAO????HAMSHIRIKIANI NAO????AU MME ONA SINEMA ZETU TU...VITU VYOTE
MNAVYO NUNUA MADUKANI VIMETENGENEZWA NA UKAWA???ACHENI SIASA ZA KIJINGA..SITAKI
UTOTO NIKITANGAZA KAZI ZANGU...KAMA HUPENDI PIGA KIMYA...
LIL WAYNE MAJANGA?. ANATAKIWA KULIPA DOLA MILLIONI MBILI.
blacktouchez.com
BAADA ya kudaiwa kuwa amepigana
chini na Mpenzi wake Christina Millian, Leo Hii tunashusha Info Mpya ya Lil
Wauyne Kuhusu kudaiwa “Mpunga” Mrefu ikiwa ni baada ya kuwepo kwa Kesi Dhidi
yake, kuhusu Private Jet (Ndege Binafs)
Mnamo Mwezi August, kampuni ya Ndege
Binafsi Nchini Marekani, SIGNATURE GROUP, walifungua Kesi dhidi ya Lil Wayne
ikiwa ni kulipwa Mkwanja Wao ambao walikuwa wanamdai Mkali huyo aliyejiengua
CASH MONEY RECORDS.
Kampuni Hiyo Ilimkodisha Lil Wayne
Private Jet Hiyo kwa ajilio ya Matumizi yake, huku akitakiwa kulipa Mkwanja
waliokubaliana, na Mwisho wa Siku mpaka July 2014 Wakati Kesi inafikishwa
Mahakamani, Weezy alikuwa anadaiwa USD Mill 1.
Lil Wayne hakulipa Chochote, na
Kadri Muda Ulivyozidi Kwenda, Ndivyo alivyokuwa akizidi kuongeza Deni Mpaka
kufikia USD Milioni 1.8 (hiyo Ilikuwa ni kufikia August ya Mwaka Huu)
USD 200,000, ambazo zinakamilisha
Idadi ya USD Million 2, ni ya kumlipa Mwanasheria.
Ingawa Weezy analalamika kuwa Hakukuwa
na Mkataba wala makubaliano wakati wa Kukodishiana Ndege Hiyo, Bado hakimu
kayatupilia Mbali Madai yake, Hivyo Piga , ua, Lazima Weezy “Atapike “ Mkwanja
Huo bila Ubishi
LIST YA WATAKAOCHUANA KATIKA TUZO ZA BET HIP HOP AWARDS 2015 HII HAPA
HATIMAYE BET HIP HOP AWARDS 2015
imeweza kumimina List ya maninja ama Wasanii kutoka Nchini marekani, pamoja na
wadau mbali mbali wa Muziki wa Hip Hop, watakaowania Tuzo hizo, ikiwa ni katika
Vipengele Tofauti.
Safari Hii itakuwa ni Msimu wa 10
Kwa BET Awards, tangia wameanzuisha Utoaji wa Tuzo hizo, na Mwaka huu,
atakayehost Mchakato Mzima, ni The Dog Father-Snoop Dogg.
“Best & Hot Female Rapper”
Kutoka YMCMB-Nicki Minaj, ameonekana Kuwa Tishio zaidi hasa kwa Kutokea Takribani
Mara Tisa Katika Category Mbali mbali ambazo zimepangwa.
Drake, Big Sean, Kendrick Lamar,
Kanye West, na Wengineo, wameonekana kuingia katika Mchuano Mkali hasa
Ukizingatia kila Mtu ana Uzito wa Kutosha Katika Mainstream.
Pia Djs, Na Website ambazo zimeweza
kusupport Muziki wa Hip Hop, nazo zimewekwa kunako Mchakato Huo.
List Hiyo ni kama Ifuatavyo:
BEST
HIP HOP VIDEO
- Big Sean featuring
- Chris Brown & Ty Dolla $Ign - "Play No Games"
- Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
- Fetty Wap - "Trap Queen"
- Kendrick Lamar - "Alright"
- Nicki Minaj featuring Beyoncé - "Feeling Myself"
BEST
COLLABO, DUO OR GROUP
- Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
- Big Sean featuring E-40 - "Idfwu"
- Fetty Wap featuring Monty - "My Way"
- Nicki Minaj featuring Beyoncé - "Feeling Myself"
- Nicki Minaj featuring Drake & Lil Wayne - "Truffle Butter"
BEST
LIVE PERFORMER
- Drake
- J. Cole
- Kanye West
- Kendrick Lamar
- Nicki Minaj
LYRICIST
OF THE YEAR
- Big Sean
- Drake
- J. Cole
- Kendrick Lamar
- Nicki Minaj
VIDEO
DIRECTOR OF THE YEAR
- Alan Ferguson
- Benny Boom
- Chris Robinson/Lil Chris
- Colin Tilley
- Director X
DJ
OF THE YEAR
- DJ Drama
- DJ Envy
- DJ Esco
- DJ Khaled
- DJ Mustard
PRODUCER
OF THE YEAR
- DJ Mustard
- J. Cole
- Kanye West
- Mike Will Made-It
- Pharrell Williams
- Timbaland
MVP
OF THE YEAR
- Big Sean
- Drake
- Future
- J. Cole
- Kendrick Lamar
- Nicki Minaj
TRACK
OF THE YEAR
- "Alright" - Produced By Pharrell Williams & Sounwave (Kendrick Lamar)
- "Blessings" - Produced By Boi-1da & Vinylz (Big Sean FEATURING Drake & Kanye West)
- "Commas" - Produced By Dj Spinz & Southside (Future)
- "Idfwu" - Produced By Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West & Key Wane (Big Sean FEATURING E-40)
- "Trap Queen" - Produced By Tony Fadd (Fetty Wap)
ALBUM
OF THE YEAR
- Big Sean - Dark Sky Paradise
- Drake - If You're Reading This It's Too Late
- J. Cole - 2014 Forest Hills Drive
- Kendrick Lamar - To Pimp A Butterfly
- Nicki Minaj - The Pinkprint
- Wale - The Album About Nothing
WHO
BLEW UP AWARD
- Bobby Shmurda
- Dej Loaf
- Fetty Wap
- Rae Sremmurd
- Tink
HUSTLER
OF THE YEAR
- Dr. Dre
- Drake
- J. Cole
- Jay Z
- Nicki Minaj
MADE-YOU-LOOK
AWARD (BEST HIP HOP STYLE)
- A$Ap Rocky
- Dej Loaf
- Drake
- Kanye West
- Nicki Minaj
BEST
HIP HOP ONLINE SITE
- Allhiphop.Com
- Complex.Com
- Hotnewhiphop.Com
- Rapradar.Com
- Worldstarhiphop.Com
BEST
CLUB BANGER
- Big Sean featuring E-40 - "Idfwu" (Produced By Dj Dahi, Dj Mustard, Kanye West & Key Wane)
- Dej Loaf - "Try Me" (Produced By Dds)
- Fetty Wap - "Trap Queen" (Produced By Tony Fadd)
- Future - "Commas" (Produced By Dj Spinz & Southside)
- Rich Homie Quan - "Flex" (Ooh, Ooh, Ooh) (Produced By Dj Spinz & Nitti Beatz)
BEST
MIXTAPE
- Future - 56 Nights
- Future - Beast Mode
- Future - Monster
- Lil Wayne - Sorry 4 The Wait 2
- Travis Scott - Days Before Rodeo
SWEET
16: BEST FEATURED VERSE
- Drake - "Blessings" (Big Sean Featuring Drake & Kanye West)
- Drake - "My Way Remix" (Fetty Wap Featuring Drake)
- E-40 - "Idfwu" (Big Sean Featuring E-40)
- Kendrick Lamar - "Classic Man Remix" (Jidenna featuring Kendrick Lamar)
- Lil Wayne - "Truffle Butter" (Nicki Minaj featuring Drake & Lil Wayne)
IMPACT
TRACK
- Big Sean featuring Kanye West & John Legend - "One Man Can Change The World"
- Common & John Legend - "Glory" (From The Motion Picture "Selma")
- J. Cole - "Apparently"
- J. Cole - "Be Free"
- Kendrick Lamar - "Alright"
PEOPLE'S
CHAMP AWARD
- Big Sean featuring Drake & Kanye West - "Blessings"
- Fetty Wap - "Trap Queen"
- Future - "Commas"
- Kendrick Lamar - "I''
- Rae Sremmurd - "No Type"
- Rich Homie Quan - "Flex (Ooh, Ooh, Ooh)"
KIMENUKA TWITTER: NI AUNT EZEKIEL TENA !!!
SIKU Ya Jana taarifa ziliznza kuzagaa kuwa, Aunt
Ezekiel, Msanii wa Bongo Muvi, ambaye alikuwa akimsupport Mgombea Urais Kupitia
CHADEMA-UKAWA, amepiga Chini UKAWA, na Kuhamia CCM.
Kwa Mujibu wa Taarifa ambazo tunazinukuu kutoka
kwa Steve Nyerere, ni kwamba Hata Vicent Kigosi- Ray, pia amejiunga na Wana
CCM.
Sasa, mapema Leo katika account yake ya Twitter,
Aunt Ezekiel ameandika kama ifuatavyo huku Baadhi ya Tweet zikimlenga
JACQUELINE WOLPER.
Wolper kasambaza uongo tumenunuliwa, mbona hasemi alipewa ngapi aje kutununua kwenda UKAWA. Sio kila kitu ni cha kufanyia usanii jamani.
— Aunt Ezekiel (@auntezeofficial) September 15, 2015
Mtanyooka tu, ukweli unachoma. Wenye namba yangu endeleeni kupiga kupata uhakika kwamba huyu ni mie. #MabadilikoNiMagufuli
— Aunt Ezekiel (@auntezeofficial) September 15, 2015
Eti Aunt Ezekiel ni nani? Nyooo! Ulivyokuwa unakenua meno wakati nakuja kwenye mikutano yenu hukuwahi kujiuliza hilo swali? #MahabaNiUlofa
— Aunt Ezekiel (@auntezeofficial) September 15, 2015
Na watawakimbia wengi. Mpaka siku @MagufuliJP anaapishwa mnaweza kuwa vipande vipande kama chipsi za Sele Bonge. pic.twitter.com/F8bY1QsSb2
— Aunt Ezekiel (@auntezeofficial) September 15, 2015
Inatosha kwa leo, maumivu yakizidi lamba hili, maana hakuna namna. #UkawaNiBiashara #MabadilikoNiMagufuli pic.twitter.com/Ah5t7DppGJ
— Aunt Ezekiel (@auntezeofficial) September 15, 2015
LUSHOTO KUTOKUPIGA KURA
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema
wananchi wa Jimbo la Lushoto mkoani Tanga, hawatapiga kura ya kuchagua mbunge
katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25.
Hatua hiyo, inatokana na kufariki dunia kwa
aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo hilo kupitia Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) kwa mwamvuli wa Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa),
Mohamed Mtoi (39). Mtoi, alifariki dunia Jumamosi iliyopita baada ya gari lake
alilokuwa akisafiria kuacha njia na kupinduka kisha kudumbukia kwenye korongo
wilayani Lushoto.
Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva,
alisema sheria inaruhusu kama mgombea atafariki dunia wakati huu wa uchaguzi
uahirishwe. “Wananchi wa Lushoto hawatapiga kura ya mbunge Oktoba 25,
tumeahirisha hadi hapo baadaye tutakapowatangazia na chama husika kitapokuwa
kimepata mgombea,” alisema Jaji Lubuva.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga,
Zubery Mwombeji, Mtoi alipata ajali katika eneo la Magamba Coast, Kata ya
Magamba wilayani Lushoto.
Alisema gari hilo lilikuwa likiendeshwa na Miraj
Nuru (43), likitokea Tarafa ya Mlola kwenda Mkuzi baada ya kumaliza shughuli za
kampeni.
Subscribe to:
Posts (Atom)