Imeelezwa kuwa moja ya mambo yanayochangia
kuanguka kwa uchumi wa Taifa ni tabia ya wizi wa fedha za umma unaofanywa na
watumishi wa Serikali kupitia njia ya manunuzi.
Hali hiyo imebainishwa juzi na Askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania (AICT) Dayosisi ya Shinyanga, Askofu John Nkola katika ibada ya sherehe za kumpongeza Mchungaji Amos Ndaki kwa kutimiza miaka 21 ya utumishi wake ndani ya kanisa hilo.
Askofu Nkola amesema kuporomoka kwa uchumi wa Taifa mara nyingi kunachangiwa na watumishi wasio waaminifu ndani ya Serikali ambao huiba fedha za Serikali kwa kutumia njia ya kudanganya kwenye manunuzi mbalimbali ya umma, hivyo kuisababishia hasara Serikali.
Akifafanua amesema vitendo hivyo vimekuwa vikifanywa na watumishi wasiokuwa na hofu ya Mwenyezi Mungu ndani ya mioyo yao, hivyo kwao dhambi ya kuiba huona ni jambo la kawaida bila kuelewa wizi wanaoufanya una athari kubwa kwa walipakodi na wananchi kwa ujumla.

EmoticonEmoticon