Ukubali ukatae, TIM TUKO MBELE Still tunakubali
sana Kila Product ya Burudani kutoka Nchini Tanzania.
SONGERA ZIGI ZIGI kwa Kitengo Chimbua Chimbua
kwa kuweza kulibaini hili na Sisi kamwe hatuwezi kuikataa Ripoti yao.
NCHI ya Kenya imekuwa ni moja kati ya Mfano
mzuri sana wa kuigwa Tangia LUPITA NYONG’O aonekane kuwa na mafanikio mazuri sana katika
tasnia ya Filamu Ulimwenguni, lakini kadri Siku zinavyozidi Kwenda, ulimwengu
wa Filamu Nchini humo unazidi kuingia katika mabadiliko mazuri na Makubwa.
TTM tumeapata nafasi ya Kucheki Kipande cha
Filamu ya PUMZI ambacho kinagharimu jumla ya Dakika 21kutoka Nchini Kenya
kikiwa kina maudhui ya Science Fiction.
Tunapozungumzia Filam za Scince Fiction,
Tunamaanisha Filam ambazo zinahusisha masuala ya Kisayansi ambayo hukushawishi
wewe mtizamaji kuamini kuwa Hilo linalofanyika hapo, ni Kweli loipo na
limetokea, ingawa huwa ni Masuala ya kibunifu.
Filamu hiyo Fupi ya Pumzi ambayo Imeongozwa na
Muongzaji Mkenya WANURI KAHIU, inazungumzia AFRIKA MASHARIKI Ijayo, Miaka 35
Baada ya Kutokea kwa Ukame wa maji ikiwa ni madhara ama Athari ya VITA KUU YA
PILI YA DUNIA.
Filamu Hii imenekana Kupendwa na wengi na Kuendana
na Uhalisia wa tamko la UMOJA WA MATAIFA (UN), kuwa Mpaka kufikia Mwaka 2030,
Kuna Uwezekano wa kuwepo kwa Uhaba wa maji Duniani kutokana na Ongezeko la
watu.
Binafsi tunadhani BONGO Moviez wanatakiwa
kutumia akili pana zaidi, kuendana na matukio makubwa ambayo hulenga Kumtokea
mwanadamu hasa katika maisha yake, tofauti na Kufikiria Ideas za kawaida tu
ambazo Ni MAPENZI kwa asilimia kubwa
EmoticonEmoticon