REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA JIJI LA MWANZA KIMEANZA RASMI LEO

6:16:00 AM


NA GEORGE BINAGI,Mwanza
Kikao cha kwanza cha baraza la Madiwani wa halimashauri ya Jiji la Mwanza, leo kimeanza rasmi huku kikitumia baadhi ya kanuni mpya, baada yam kikao hicho jana kushindwa kufanyika ili kupisha semna kwa wajumbe wa baraza hilo juu ya kanuni hizo mpya zitakazotumika kuliongoza baraza hilo.

Miongoni mwa kanuni mpya ambazo zimeingizwa na TAMISEMI katika vikao vya halimashauri zote hapa nchini ni pamoja na kila diwani kuandaa na kuwasilisha mbele ya baraza taarifa ya utekelezaji wa shughuli za maendeleo ya Kata yake kabla ya kikao cha baraza kuanza.

Kanuni nyingine ambazo ni mpya zinahusu dua maalumu ya kuiombea halimashauri na kuimba wimbo wa Taifa kabla ya vikao vya baraza la madiwani wa halimashauri kuanza, sanjari na maswali ya papo kwa hapo kwa mwenyekiti wa baraza la madiwani ambae ni Mstahiki Meya, ama kwa Mtendaji wa baraza ambae ni Mkurugenzi wa Jiji.

Kutokana na kanuni hizo mpya, wajumbe wa baraza la madiwani waliafikiana hiyo jana kusitisha shuguli za kikao cha kwanza cha baraza hilo ili kupata semna kuhusiana na kanuni hizo ili kuwajengea uwezo na uelewa katika kuzitumia.

Kwa mantiki ,Kabla ya kikao cha leo kuanza Redio Metro ilizungumza na baadhi ya madiwani ambao ni wajumbe wa baraza hilo la madiwani wa halimashauri ya jiji la Mwanza ambao wameeleza kwamba baada ya semna ya jana waliafikiana kwa pamoja katika kutumia kanuni hizo mpya.

Baada ya kupata ufafanuzi huyo nje ya Ukumbi wa halimashauri ya Jiji la Mwanza, uliwadia wakati wa kikao hicho cha baraza la Madiwani kuanza, ambapo tulishuhudia kanuni mpya zikianza kutumika rasmi, na hapa Mwenyekiti wa baraza hilo ambae ni Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza Stanslaus Mabula aliwaongoza wajumbe katika kuimba wimbo wa Taifa pamoja na dua maalumu ya kuimbea halimashauri kabla ya kikao kuanza rasmi kama kanuni zinavyoelekeza.

Baada ya wimbo wa Taifa na Dua kwa halimashauri, mwenyekiti alitoa mwongozo wa ajenda ya kwanza ya kikao ambayo ni wajumbe wote kuzingatia suala la mavazi ambayo ni ya heshima sanjari na majoho huku akibainisha kuwa mavazi na kofia za aina yoyote havitaruhusiwa katika vikao hivyo.

Ajenda iliyofuata ilikuwa ni madiwani kuwasilisha taarifa za shughuli za maendeleo katika kata zao ikiwa ni utaratibu mpya kabisa kwa kuwa hapo awali utaratibu huo haukuwepo, hali ambayo mwenyekiti amebainisha kwamba imepelekea madiwani kuwasilisha taarifa zenye mapungufu na hivyo mwenyekiti kutoa pendekezo la kuwepo kwa semna elekezi juu ya namna ya kuandaa taarifa hizo ambazo zitakuwa zikitolewa kila baada ya miezi mitatu.


Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER