REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

EMINEM AZUNGUMZIA KITENDO CHA 50 CENTS KUONDOKA KATIKA LEBO YAKE.

5:40:00 AM

KITENDO Cha 50 CENTS Kuondoka Shady Records, Aftermath Entertainment na Iterscope Records, Zimewastua Wengi sana ambao walikuwa wanafahamu uhusiano mzuri na wa karibu baina ya 50 Cents Mwenyewe, Eminem na Dr.Dre.
Lakini baada ya Kutoa Taarifa hapo jana Kuwa ameamua Kutemana na Kampuni hizo ambazo ndizo zimemtoa katika Music Industry Ulimwenguni kote na Kufikia hapo alipo hivi sasa, Mmoja kati ya Wamiliki wa Lebo hiyo ambayo ilikuwa ikimsimamia 50 Cents na kazi zake kwa Muda sasa, EMINEM, amesema kuwa anajivunia Kumfahamu 50 Cents, na Kitendo cha yeye kuondoka kwao, hakitaathiri Urafiki wao wa muda Mrefu.
Aidha Emenem ambaye pia anafahamika kwa jina la Slim Shaddy, amesema Kuwa, yeye pamoja na SHADY RECORDS, wanajivunia Kuwa sehemu ya Mchango wa Mafanikio ya 50 Cents katika Muziki.
Tofauti na hapo, Eminem aliongeza kuwa, Kama isingekuwa uwepo wa 50 Cents katika Studio Hizo, basi hata Shady Records isingekuwepo hapo Ilipofikia.
Kwa Upande wake 50, amesema kuwa amekuwa na Muda Mzuri sana wakati akifanya kazi na Shady/Aftermath/ na Interscope Records, huku akiwashukuru sana Dr. Dre na Eminem maana amejifunza Mengi kutoka Kwao. Lakini hivi sasa anahitaji kwenda sehemu Nyingine na Kujifunza Mtazamo Mpya.
50 Cents anaelekea katika Studio za Caroline,iliyotokana na CAPITOL RECORDS.

Ingawa Hivi sasa anajiandaa kushusha Albam yake Mpya ya THE ANIMAL AMBITION, Albam ya GET RICH OR DIE TRYING ambayo ilikuwa na Mikwaju kama Vile IN DA CLUB, MANY MENT, P.I.M.P, ilisukwa Vizuri na Lebo ambayo anatemana nayo

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER