G-SENGO BLOG
KIKUNDI
cha Wanaume wapiga kasia cha Costantine Lusalage kutoka Sengerema Mkoani Mwanza
kimeibuka na ubingwa wa Mkoa wa fainali za kimkoa mbio za mitumbwi chini ya
udhamini wa bia ya Balimi Extra Lager zijulikazo kama “Balimi Boat Race 2014”
na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 900,000/= pamoja na tiketi ya
kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za Kanda zinazotarajiwa
kufanyika Desemba 6 mwaka huu jijini Mwanza.
Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha
Elisha Jacob kutoka Misungwi ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
700,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini
Mwanza pia, wakati nafasi ya tatu ilichukuliwa na kikundi cha Emmanuel
Masanyiwa kutoka Luchelele ambacho kilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 500,000/=
na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Daniel Genha kutoka Misungwi
ambacho kilizawadiwa Shilingi 400,000/=
Nafasi ya tano hadi ya tisa walipewa kifutajasho
cha pesa taslimu Shilingi 250,000/= kila kikundi ambavyo ni kikundi cha Mussa
Msalaba kutoka Sengerema, Joseph Jacob kutoka Misungwi, Katula Msese kutoka
Kigoto, Faustine Daud kutoka Ibanda, Lubongeja Manyasiwa kutoka Sengerema na
Simon Salala kutoka Misungwi.
Upande wa Wanawake kikundi cha Joyce Alon kutoka
Misungwi kilifanikiwa kutwaa ubingwa na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi
700,000/= pamoja na nafasi ya kuwakilisha mkoa katika fainali za Kanda jijini
Mwanza.
Nafasi ya pili Wanawake ilichukuliwa na kikundi
cha Tabu Daudi kutoka Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 600,000/=,washindiwa
tatu ni kikundi cha Ntabo Hussein kutoka Luchelele ambao walizawadiwa Shilingi
400,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na kikundi cha Leah William kutoka
Misungwi ambao walizawadiwa Shilingi 300,000/= na nafasi ya tano hadi ya kumi
walizawadiwa kifuta jasho cha Shilingi 200,000/= kila kikundi ambavyo ni
kikundi cha Winifrida William kutoka Misungwi, Revina Magafu kutoka Kigoto,
Anna Elias kutoka Kigoto, Moshi Maji kutoka Kigoto, Kizuka Kapani kutoka Bwiru
na Robby Mwita kutoka Mwaloni.
Akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi Meneja wa
bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa kwanza alishukuru vikundi vyote
vilivyojitokeza kushirika mashindano hayo lakini pia aliwapongeza wale wote
waliofanikiwa kupata zawadi na kuwaomba waliofanikiwa kupata nafasi ya
kuwakilisha Mkoa wa Mwanza kwenye fainali za Kanda wafanye mazoezi ya kutosha
na mwisho wasiku ushindi ubaki Mwanza kwa mwaka 2014.
Edith alisema washiriki wote mliofanikiwa kupata
zawadi mkatumie vizuri hizo pesa kwa maendeleo yenu na pamoja na maadalizi ya
mashindano mengine mwaka ujao.
Fainaliza Kanda zambio za mitumbwi zijulikanazo
kama “Balimi Boat Race 2014” zinatarajiwa kufanyika Desemba 6, mwaka huu jijini
Mwanza katika ufukwe wa Mwaloni.
EmoticonEmoticon