MKALI WA “KABUMBUMBU” kunako klabu
ya Totenham nchini Uingereza Emmanuel Adebayor amekosana na mamaake kwa madai
kwamba anatumia uchawi kumharibia kazi yake.
Lakini mchezaji huyo wa zamani wa kilabu ya
Arsenal anadai kwamba mamaake aliondoka mwenyewe na kwamba hawana mawasiliano
yoyote kati yao kwa kuwa amekuwa akitumia uchawi kutaka kumuharibia kazi yake.
'' Ninawezaje kuzungumza na mama ambaye yeye na
dadaangu wamekuwa wakijaribu kuniroga''
Mchezo wa Adebayor katika kilabu ya Tottenham
umeathirika katika kipindi cha miezi kadhaa iliopita huku Tottenham ikidaiwa
kujaribu kumuuza kwa mkopo mchezaji huyo katika dirisha la uhamisho mnamo mwezi
January kufuatia kushuka kwa mchezo wake.
EmoticonEmoticon