BBC SWAHILI
Daktari wa Marekani aliyekuwa
akiwahudumia wagonjwa wa Ebola Nchini Guinea amepimwa na kukutwa na virusi vya
ugonjwa huko katika hospitali ya ya mjini New York.
Dr Craig Spencer ambaye ni mmoja
kati ya madaktari wasio na mipaka alianza kujisikia maumivu na homa siku chache
tu baada ya kurejea Marekani akitokea Afrika Magharibi.
Siku ya Alhamisi wiki hii Craig
alipelekwa hospitali kwaajili ya vipimo na kisha akatengwa kwa uchunguzi zaidi
wa afya yake.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya
habari Meya wa mji wa New York Bill de Blasio amesema watu hawapaswi kuwa na
hofu kwani hatua zote mhimu zilifuatwa katika kumchunguza Dr.Craig na hadi
alipobainika kuwa na maambukizi hayo.
Kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa
wa Ebola kwa Dr.Craig kunaongeza idadi ya waliobainika kuwa na ugonjwa huo
nchini Marekani kutoka watatu na kufikia wagonjwa wanne.
EmoticonEmoticon