KUNA tetesi ambazo zimeanza kuzagaa
kuwa Nick Cannon na Mkewe Mariah Carey wameshaingiliwa na Kidudu Mchepuko, hali
ambayo inaweza kuleta athari kubwa katika Ndoa yao.
Kitengo Chimbua Chiombua, kimenyaka
Mchakato Mgumu kweli kuutabiri, na kudai kuwa, kumekuwa na Ugomvi wa hapa na
pale baina ya wanandoa hao wawili huku sababu ikiwa ni tuhuma za kuchepuka
zinazomkabili Nick Cannon.
Aidha Mtonyo haujaishia hapo tu, pia
inasemekana Nick Cannon hivi sasa amehamishia Maskani ya Muda, katika Hotel
moja hivi ambayo bado hatujalinyaka Jina
Tofauti na Hilo, Pia Kuna mmoja wa
Ndugu wa karibu kwa wanandoa hao, ambaye alidai kuwa, Mariah carey amechoshwa
na Suala la Mchepuko ambalo mara Nyingi
amekuwa akilifanya Nick Cannon, hali ambayo imemfanya amuwekee walinzi
ambao watazuia warembo wote wanaomsogelea Nick, hali ambayo ilidhihirika Katika
POOL
PARTY moja iliyofanyika Las Vegas, huku Nick Cannon
akiwa ni MC wa Shughuli hiyo.
Mariah na Nick walifunga ndoa mwaka
2008, na Mpaka Hivi sasa bado wanamaisha yao katika Ndoa Hiyo, licha ya Mariah
Carey kutokufanya Vizuri katika Muziki kama ilivyokuwa awali.
EmoticonEmoticon