USIKU wa kuamkia Jumapili ya Leo, majira ya Saa
3:34 Usiku, Soko Tegemezi la Mtaa Wa Bugarika,Jijini Mwanza almanusura
Liteketee kwa Moto Baada Duka Moja Kushika Moto na Kusababisha Maduka Mengine
Mawili Kuanza Kushika Moto.
Mpaka Mwandishi wa BLACK TOUCHEZ anafika Eneo la
Tukio, Moto Ulikuwa bado unapamba Moto huku Hofu kubwa ya Wakazi wa Mtaa Huo,
ni Mashine ya Kusaga, ambayo Ilianza Kushika Moto katika Paa Lake.
Kwa Mujibu wa Taarifa kutoka Kwa Mashuhuda
waliozungumza na BLACK TOUCHEZ, wanasema kuwa, Awali ulisikika Mlipuko Mkubwa
Kutoka katika Duka Hilo, na Kusababisha PAA la Duka Kufumuka kwa Kasi ya Ajabu.
“Baada ya Kusikia Mlipuko huo wa Kwanza, Ghafla
Tulisikia Mripuko Mwingine Tena, ambao ulifumua Paa Hilo Moja Kwa Moja na Moto
Kufumuka kwa Kasi” alisema Shuhuda aliyejitambulisha kwa Jina la KULWA.
Baada ya Jitihada za Dhati Kufanyika, hatimaye
Gari la Zima Moto liliwasili Eneo la Tukio na Kufanikiwa kuokoa Robo tatu ya
Mali za Wafanya Biashara ambao Wana maduka Katika Eneo Hilo.
HATA hivyo, Mpaka Hivi sasa, Taarifa Zinaeleza
kuwa, Hakuna Mtu aliyepoteza Maisha katika Ajali Hiyo, ingawa kuna watu wawili
(Mume na Mke)b ambao wamejeruhiwa, wakiwa katika Hatua za Kufunga Duka lao,
ambalo lilipata Shoti ya Umeme
EmoticonEmoticon