Mchungaji Christopher Mtikila amefungua kesi
kumshitaki Askofu Dk. Valentino Mokiwa wa Anglican.
Msingi wa kesi ni kwamba Askofu Mokiwa alimshika
makalio Mtikila na kwamba kitendo hicho kilichotokea Juni 25 mwaka jana
walipokutana maeneo ya Ilala, kimemdhalilisha.
Mtikila alikuwa ameitwa na Askofu kujadili tamko
la la Mtikila kwamba Kanisa la Anglican linajihusisha na ufisadi, ukiwemo
ufisadi wa au wizi wa vifaa vya Hospitali ya Mission ya Millo iliyoko Ludewa
mkoani Iringa.
Mtikila alivyoitwa na Askofu kujadili hilo
alifika na wenzake watatu wa taasisi ya Liberty International Foundation na
wakakaribishwa kwenye moja ya jengo la dayosisi ya St. Nocholas, usiku wa saa
03:00.
Muda mfupi baada ya kikao kuanza, Askofu Mokiwa
ambaye alikuwa na wenzake saba, alisimama na kuwataka wajumbe wote wakaguliwe
kama kuna mtu ana kinasa sauti, kazi ambayo aliifanya yeye baada ya kufunga
mlango.
Katika upekuzi huo ndipo tuhuma hizo
zilipopatikana kutokana na madai kwamba operesheni hiyo ilienda mbali zaidi ya
lengo la kawaida.
"Mlalamikiwa alitangaza kuwa, kila mtu
aliyekuwemo kwenye mkutano lazima apekuliwe na kwamba atakayekataa angetumia
nguvu, kwa kuwa alikuwa na bastola, hakuna aliyebisha.
Alianza kupenyeza mikono yake kwenye shingo
kuelekea chini kisha huko chini mikono ya mlalamikiwa ilionekana waziwazi
ikipepesa sehemu za siri za mlalamikaji".
Mchungaji Mtikila ameiomba Mahakama imwamuru
Askofu Mokiwa alipe fidia ya shs. bilioni moja kwa kumdhalilisha. Madhara zaidi
ya kitendo hicho ni pamoja na mfadhaiko, masikitiko, wasiwasi, aibu katika
jamii na kupata shinikizao la damu la mara kwa mara na matatizo ya moyo
Kesi inataarifiwa kuwa kwenye Mahakama ya
Kisutu, chini ya Hakimu Mchome
CHANZO: AMANI (UKURASA WA 2 & 3)
EmoticonEmoticon