Rais wa Misri Abdel
Fattah al-Sisi ameliambia gazeti moja nchini humo kuwa aanajutia uamuzi wa
mahakama kuwafunga jela wandishi wa tatu wa shirika la habari la Al Jazeera.
Bwana Al Sisi amesema
kuwa waandishi hao watatu walipaswa kuamrishwa kurejea makwao badala ya
kuhukumiwa kifungo jela.
Kwenye mkutano na
wandishi habari rais Al-sisi alisema kuwa kuhukumiwa kwa waandishi hao
kumeonyesha picha mbaya kuhusu Misri.
Waandishi hao
walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 7- 10 gerezani kwa kueneza habari za
uongo na kulisaidia kundi lililopigwa marufuku la Muslim Brotherhood.
Muda mfupi baada ya
hukumu hiyo rais Al sisi alisema kuwa hawezi kuingilia shughuli za mahakama
Al Sisi amesema hukumu
hizo zilitoa picha mbaya kuhusu Misri
Lakini matamshi yake ya
hivi punde yametoa matumaini kwa familia za mwaandishi wa habari raia wa
Australia Peter Greste na mwenzake mwenye asili ya Canada na misri Mohammed
Fahmy
Nduguye Peter Greste
Andrew amesema kuwa matamshi hayo yamempa matumaini.
Naye nduguye Mohammed
Fahmt amesema kuwa hii ni ishara kwamba jambo fulani ni lazima lifanywe.
Lakini familia ya
mwandishi mwingine wa tatu aliye kizuizini Baher Mohammed ilipuunza matamshi
hayo na kuyataja kuwa ya kuchekesha.
Waandishi hao wote watatu
wanajipanga kukata rufaa
EmoticonEmoticon