Licha ya Ugumu wa Mazingira Yetu hasa Sie Watoto wa Uswahilini, lakini kubali, ukatae, hata akina MRISHO NGASSA, wametopkea Huku, hii Ndiyo Burudani Yetu |
Tunauwezo Mzuri wa kukabiliana na Adui zetu wanathubutu kunyemelea Magoli Yetu, ingawa hatuna Nyavu |
VIWANJA vyetu havina Nyasi, lakini Vumbi na Michanga, ni Nyasi tosha, ilimradi tu, tunapata Burudani, kipaji kinaonekana, uzoefu unaongezeka, na Siku Inaenda |
Hatuna Uwezo wa kununua Viatu. Na hata Hivyo, Raha ya "Kabumbu" letu, ni kulisukuma bila Viatu wala Socks |
Kuna baadhi ya Sheria za Soka huwa hazifuatwi katika Soka Letu sisi watoto wa USWAZZ, lakini baadhi kama PENALTY, CORNER KICKS, FOULS, na HAND TO BALL, tunaziona saaana, maana tunahitaji Ushindi |
Huwa hatubagui watizamaji ama mashabiki. Mara Nyingi hutupa Motisha japo ni wachache |
Jezi Zetu mara Nyingi huwa ni Arsenal, ama Machester United na Timu Nyinginezo za Ligi ya Uingereza. Tukiona hivi, basi tunaamini ipo siku nasi tutacheza Ligi kubwa kama hao Wengine |
Tunajua Mwanza kuna Mawe, Lakini hata siku moja hayatuzuii kusakata Soka letu, ingawa ni hatari hasa kujikwaa, ama unapoanguka katika Jiwe Hilo |
Tunatamani Serikali za Mitaa zitutengenezee Viwanja Vizuri vya kucheza Soka huku Uswaz Kwetu, lakini ni Ndoto kwa kweli |
Sio Mawe Tu, Viwanja Vyetu vinakabiliwa na Miti hatarishi iliyokauka, Chupa zinazoweza kudhuru miguu yetu maana hatuchezi na Viatu, pamoja na Mazingira Salama Kiafya |
EmoticonEmoticon