Aisee, Hii inaweza kuwa ajabu ya
aina yake hasa kwa waleambao wamekuwa wakifuatilia Mahusiano ama mahaba ya
Mkali wa HIPS DON’T LIE, Shakira, pamoja na Mchezaji wa BARCELONA, Gerald Pique
mwenye Miaka 27..Sikiliza kwa Umakini Mtinyo Huu,
Shakira ameweza kuushangaza Umati wa
watu tofauti alipotoa kauli ya kuonekana kutokuwa na Mpango wa Kufunga ndoa na
Boyfriend wake huyo wa Muda Mrefu.
Akizungumza kwa ufafanuzi kuhusu
kauli yake, Shakira mwenye Umri wa Miaka 37, amesema kuwa hivi sasa hafikirii
suala hilo la Ndoa kwa hivi sasa, kwa sababu haitaleta Utofauti wa Aina yoyote
katika mahusiano, na bado itabaki kuwa vile Vile.
Aidha Shakira ambaye Mnamo March
alikamilisha Albam yake ya 10 aliyoipa Jina la SHAKIRA, ameongeza kuwa, hivi
sasa wameshafanikisha kile ambacho wanacho, maana wanapendana kwa Dhati, Wana
Mtoto, Uhusiano wao tayari umeshakuwa Mzuri na wenye mafanikio, hivyo suala la
Ndoa halitobadilisha Chochote katika masuala hayo Muhimu ambayo wamesha yapata.
Tofauti na Hilo, Shakira alipoulizwa
kuhusu sala, ama kitu kinachomfanya awe “happy” siku zote, alesima kuwa ni
kushare kila alicho nacho na Mtoto wao Milan, ambaye hivi sasa ana Miezi 17,
ukizingatia anapenda kumfundisha kitu kipya Kila Siku
EmoticonEmoticon