NEW
YORK , Marekani.
KAMA Utakuwa huchezi mbali na TTM, basi utakuwa
unafahamu vizuri kabisa kuwa rapper Kanye west hapatani hata Kidogo na
Mapaparazi, sasa Kuna hili Toka Chimbua Chimbua.
Kubali Ukatae Kanye West ameshaanza kuwa na
mashaka mazito juu ya Usalama na Mtoto wake NORTH WEST baada ya kuonekana sana
hadharani katika Kipindi cha Mchakato wa kufunga Ndoa, ambao ulihitimishwa
Mwezi Uliopita.
Kwa mujibu wa chanzo kilichopo karibu na
Wanandoa hao, Kimedai kuwa, Kanye West na Mkewe Kim kardashian wamekuwa
wakibishana sana na hata kukwaruzana kuhusu Ishu ya Mtoto wao kuonekana hadharani
na kupigwa picha Ovyo na Mapaparazi, jambo ambalo Kanye hapendi na
walishakubaliana Awali kuwa tukio hilo lisifanyike hata kidogo.
Aidha Kanye alimchana Kim Kardashian kuwa, Hivi
sasa Mchakato wa Ndoa umeisha, Hivyo haturuhusu Mtoto wake aonekane hadharani
hata kidogo, na hata Picha zake hazitakiwi kuzagaa Mitandaoni Bila Idhini yake
ama sababu maalum.
Tofauti na Hilo, Pia Yeezy amepiga marufuku
North West kuonekana katika Kipindi cha KEEPING UP WITH THE KARDASHIANS,
kinachoongozwa na Kim Mwenyewe.
EmoticonEmoticon