Nay Wa Mitego anasherehekea siku yake ya
kuzaliwa leo (June 9) na kufanya sherehe ya kwanza ya kusherehekea siku hii kwa
kuwa hakuwa na utaratibu huo.
Nay amesema kuwa ameamua kufanya sherehe hiyo
kwa kuwa mwaka huu kwake ni tofauti na miaka mingine kwa kuwa amepiga hatua
kubwa sana katika maisha kupitia muziki wake hivyo ameamua ajipongeze kwa
hafula fupi.
Mara nyingi kibongobongo watu huficha umri pale
wanapofanya sherehe za siku ya kuzaliwa, utaambiwa tu ‘nimeongoza mwaka
mmoja…nina miaka mingi…’, lakini hii ni tofauti kwa True Boy Nay wa Mitego
ambaye ametaja umri wake bila kuficha kutokana na furaha aliyonayo.
“Leo natimiza miaka 29 labda niwaambieni. Kwa
wale ambao walikuwa hawajui mimi sio mtu wa kuficha mimi ni niko live siku
zote.” Amesema Nay.
“Leo natimiza mwaka wa 29 nashukuru, Mwenyezi
Mungu amjalie miaka mingi mama yangu aendelee kuwepo aone mafanikio yangu. Na
kingine, leo ni siku yangu ya furaha sana ntakuwa nasherehekea nikiwa home na
washikaji zangu wawili watatu.” Ameongeza.
Nay ameendelea kuonesha utofauti kwa kuwa
ameamua kujinunulia zawadi ya gari la kifahari (kibongobongo) ambalo
linagharimu shilingi milioni 36.
“Nimejinunulia gari aina ya Murano nafikiri ndio
gari yangu ambayo leo ntakuwa nayo na ndio birthday yangu. Inagharimu milioni
36, hii ni ya mwaka 2007…bado mpya bado inadai. one love kwa mashabiki wangu.”
Ameeleza Nay wa Mitego.
EmoticonEmoticon