Unaweza Ukadhani ni kituko ama Kitu cha
Kuchekesha, lakini Ukweli ni Kwamba, watoto wawili nchini Uganda, wameishi
maisha yao yote mpaka hivi sasa,bila kuota Nywele wala Meno.
INNOCENT KYALIMPA Mwenye Umri wa Miaka 10, na
AMBROSE MUGISA mwenye Umri wa Miaka 12,
hivi sasa ni Wanafunzi wa darasa la Tatu katika Shule ya Msingi Kitwara, na Ni
wakazi wa kijiji cha Kampundu, Kilo Mita 15 Kutoka Mjini Kiryandongo, Uganda.
Watoto hao wanaishi na Bibi yao Ngoziwe, ambaye
amekuwa nao tangia mama yao Mzazi alipowatelekeza, huku Wakikutana na
Changamoto tofauti ikiwemo Kutengwa, Kutukanwa, pamoja na Kuathiriwa na Mionzi
ya Jua.
Kwa mujibu wa Mtaalamu wa masuala ya Ngozi
Nchini Uganda, Dk. FRED KAMBUGU, amesema kuwa tatizo hilo ni la Kurithi ambalo
Kisayansi huitwa congenital ectodermal dysplasia (KONJENITO EKTODEMO
DAISPLASIA), na husababisha Mtu kutokuota Nywele, Meno, Kucha na Mengineyo.
Watoto hao wawili hawana Uwezo wa Kula chakula
Kigumu, huku wakijitahidi kukwepa Jua ili wasiumie
CHANZO: NEW VISION
EmoticonEmoticon