PROFFESOR JAY-JOSEPH HAULE
“Sisi kama mabalozi wa Ansaf tulikabidhi saini
za wakulima, kuna kituo kimoja cha radio kinaitwa Farmers Radio, kilifanya
research na wakawatembea wakulima kadhaa, sehemu tofauti tofauti na kuangalia
wakulima wanamatatizo gani na nini kifanyike ili kuwasaidia wakulima wa Tanzania
na Afrika nzima kwa umoja , so mimi kama balozi jana nilichokifanya nilikabidhi
signature za wakulima wa Tanzania zaidi ya milioni 2 , kwa mweshimiwa Rais
Kikwete ambao wengi waliweka matatizo yao ,wameweka hoja zao ambazo
zinawakabili ili kwa upande wa serikali waweze kuzifanyia kazi na pia kumwagiza
Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haende kuliongea hili katika
mkutano mkuu wa Afrika , 2003 walikuwa wanadhamira ya kuwekeza kwenye kilimo,
na mwaka huu 2014 umechaguliwa kama mwaka wa kilimo kwaiyo Rais atakuwa huko
Maputo Msumbiji baadae ,wanamkutano wao , pia tumemwagiza Rais akaliongelee
hili swala la changamoto za wakulima wadogo wa Tanzania na Afrika
nzima’’
AY-AMBWENE YESAYA
“Cha msingi lazima tufanye juu chini kilimo kiwe
juu, kwaiyo Tanzania ni mojawapo ya nchi ambazo hazichangiti asilimia kumi
kwenye kila bajeti ya mwaka kuwekeza kwenye kilimo, kwaiyo ule ujumbe unatakiwa
umshawishi Rais, kuanzia mwaka huu wawe wanatenga asilimia kumi au zaidi ya
asilimia kumi kwajili ya kuwezesha sekta ya kilimo, kingine ni kwamba ku,motivate
vijana kwenda kwenye kilimo kwa sababu kilimo kinakaa kama nicha watu masikini
au kama cha wazee, wakati vijana tukiweza kujikita kwenye kilimo mpaka kufika
2030 tutakuwa tupo mbali sana, kwaiyo ujumbe wangu nilimkabidhi Rais akaupokea,
na akatoa speech yake, akasema ujumbe umefika, Pia akasema kabla ata hajaenda,
kwa sababu anamkutano huko Malawi na Equatorial Guinea juni 25 mpaka juni 27
,atapeleka ujumbe kwa wahusika na litashughulikiwa”
EmoticonEmoticon