REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

WIZI BADO UNAITAFUNA INDUSTRY YA MUZIKI ULIMWENGUNI..THIS TIME YAMEKUTA DJ KHALEED

2:19:00 AM

Mbwadidi la Wizi hasa wa Idea kunako Music Industry bado linazidi kushambaa huku likionekana kuwatafuna zaidi Wasanii Wakubwa ambao tayari wana majina na Heshima yakutosha kunako Music Industry ulimwenguni Kote.

Siku ya Jana TTM tulikupa Mtonyo kuhusu Furaha ya DJ KHALEED kufanya Collable kwa Mara ya Kwanza na JAYZ katika Ngoma yake Mpya ya THEY DON’T LOVE YOU NO MORE, huku akidai kuwa amepokea Baraka tele toka kwa watu mbali mbali ambao wanamfahamu vizuri Jay z, hasa kutoka Mitaa ya BROOKLYN ambako amekulia.

Lakini Kitengo cha Chimbua ambacho kinaaminika ndani ya TTM, kimeshusha Ripot Nyingine kuwa Huenda Ujio wa Track hiyo ukaanza kwa Mkosi wa hali ya Juu baada ya DJ KHLAEE kudaiwa kuwa ameiba IDEA ya COVER ambayo inatumika kuutambulisha na Kuupa Promo Wimbo huo.

Ripoti hiyo imedhihirisha kuwa Rapa Mmoja Nchini Marekani anayefahamika kwa Jina la KOLLEY, ndiye ambaye yuko katika Mchakato wa Kumfungulia Mashtaka DJ KHALEED, kwa Madai ya Kutumia Idea ya COVER yake, aliitumia katika Mixtape yake ya REAL NECCAH THING (REAL NIGGA SHIT) ambayo aliiachia Wiki 6 Zilizopita
Kama utakuwa ni Mfuatiliaji Mzuri kunako Mitandao Mbali mbali, 

Mchakato Mzima Ni Kwamba, COVER ya KOLLEY inamuonesha akiwa ameng’ata Cheni ya Dhahabu kwa Kutumia Meno yake ya Dhahabu, wakati DJ KHALEED naye akionekana amefanya Hivyo Hivyo.

Hata Hivyo, Bado Mabadiliko yoyote hayajafanyika na Dj Khaleed hajazungumza chochote

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER