REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

USHER RAYMOND KUMRUDISHA CHRIS BROWN KWA MAFANZ WAKE.

2:47:00 AM

Wengi Tunafahamu kabisa kuwa Brown Breezy hivi sasa Yuko Jela akisubiri Kesi yake na hukumu kwa makosa kadhaa aliyoyafanya ikiwa ni pamoja na kumfumua Mangumi Jombaa mmoja aliyejitokeza kunako Zoezi la Upigaji picha bila Idhini yoyote.

Baada ya TTM kuzama kunako info za NYUMA YA PAZIA, tumeweza kunyaka Mtonyo kuwa, Muimbaji Mkongwe hasa kunako mahadhi ya RnB, USHER RYMOND,  amesema kuwa, amemshirikisha Chris Brown katika Albam yake mpya, na mashabiki wake wanatakiwa kusikiliza Ukali uliopatikana katika Track Hiyo.

Usher alifafanua kuwa, Ngoma ambayo wameifanya (yeye Na Breezy), inajibu maswali mengi sana ambayo wengi wamekuwa wakijiuliza.

Pia ameongeza kuwa, Track hiyo inafafanua namna ambavyo Binadamu tunakutana na Magumu Mengi, lakini ukweli utabaki kuwa pale pale kuwa sisi ni Binadamu, na Tuna Mengi ambayo tunatakiwa kupitia.


Tofauti na masuala ya Track, Pia Mkali huyo wa DJ GOT US FALLING IN LOVE,amesema kuwa hajakutana mara kadhaa na Chris Brown tangia ameingia Jela, ingawa baada ya Kutoka Rehab, na anaamini kabisa kuwa baada ya yote yanayomkabili, Atabadilika na kuwa bKijana Mwema

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER