Kama ambavyo tumeweza
kukuambia jana, moja kati ya watu ambao wanatafunwa na Mbwadidi la Wizi wa
Nyimbo, Idea, Beats na kadharika, ni wasanii wakubwa, tena wenye Majina na
Heshima Kubwa tu, kunako music industry Ulimwenguni Kote
Baada ya jana kukupa
Mtonyo kuwa DJ KHALEED yuko kunako Msala Mzito wa kuiba idea ya Cover ya Msanii
Mwingine na Kuitumia, This Time TTM tumenyaka Nyingine kuwa Kuna Mfungwa Mmoja
ambaye amewafugulia mashtaka JAY Z, KANYE WEST na RIHANNA kwa Madai ya kuibiwa
Ngoma Yake.
Unaweza ukajiuliza
kuwa Mchakato huo Ukoje, ila kwa Mujibu wa data za kutosha kutoka Kunako
KITENGO CHIMBUA CHIMBUA, inasemekana kuwa Mfungwa Huyo kutoka Jijini CALIFONIA,
anayefahamika kwa Jina la RICHARD DUPREE, anaweza kuwa mmoja kati ya Waandishi
wa Nyimbo wa Kuogopwa katika Karne Yetu,
baada ya Kudai kuwa, JAY Z, KANYE WEST, RIHANNA, BEYONCE na CHRIS BROWN
wamemuibia Baadhi ya Nyimbo kati ya Mikwaju 3000 aliyoiandika akiwa Jela.
Kwa Mujibu wa Maelezo
ya Mfungwa Huyo, Amesema kuwa kutokana na Wizi huo ambao anauhakika nao kabisa
ikiwemo Ngoma ya RUN THIS TOWN ya Jay Z, Kanye West na Rihanna, amefungua
Mshtaka ya Madai ya Fidia katika Utumikaji wa Mikwaju yake bila Idhini yake, na
Kiasi ambacho anahitaji ni USD MILLION 2.4, ingwa haitakuwa kazi rahisi kwake
kuzipata hasa katika kipindi hiki.
Lakini KITENGO CHIMBUA
CHIMBUA kimezidi kumimina Ripot kuwa, Dupree anadai kuwa Njia ambazo Zilitumika
kuiba Nyimbo zake ambazo alikuwa akiziandikia GEREZANI, ni Mashirika ya
Kiusalama Nchini Humo, CIA,JESHI LA POLISI na FBIYONCE kupata Nyimbo hizo.
Mashtaka hayo
yamefunguliwa katika Mahakama ya Mashariki Mwa CALIFONIA, mnamo APRIL 21
EmoticonEmoticon