RAPPER WAKAZI ANA MPANGO WA KUMILIKI STUDIO YAKE
BINAFSI ITAKAYOMSAIDIA KUREKODI NYIMBO ZAKE KWA MUDA ANAOTAKA KUFANYA HIVYO
BILA KUSUBIRISHWA.
TTM imezinyaka kuwa ameamua kufanya hivyo kwa kuwa
anataka kufanya albam zake hivyo anataka kuivuka changamoto inayotokana na
kufanya kazi katika studio mbalimbali za watayarishaji wenye ratiba zao
binafsi.
“Moja kati ya vitu muhimu sana ni hiyo kwamba
kuhakikisha kwamba ninatoa albam. Na mimi ninavyoona kwenye process ya kurekodi
albam unakuwa unazunguka katika maproducer mbalimbali kwa nia ya kuweka vitu
sawa. Halafu ukusanyaji wa kazi zako inaweza kuwa headache.” Amesema Wakazi.
Changamoto ya kuibiana idea na kazi ni sababu
nyingine inayomsukuma Wakazi kuwa na studio yake.
“Na vilevile siku hizi kama unaona sijui mtu
kaibiwa idea mara nini…kwa sababu kazi tunaziacha kwa watu mbalimbali, hujui
nani atakuja kusikia nani anafanya nini. So, cha muhimu nikawa nasema nikiwa na
studio mimi mwenyewe namaanisha kwamba ntakuwa nacontrol kitu gani cha kufanya
saa ngapi na lini nahikikisha kazi zote ziko tayari na itakuwa rahisi mimi
kuzikusanya kazi zote na kuziweka katika CD moja kuhakikisha mashabiki wangu
albam wanazipata katika siku ambayo nikisema inatoka.” Ameeleza.
Amesisitiza kuwa anahitaji studio yake iwe
imekamilika mwaka huu na kwamba sapoti ya mashabiki wake kununua kazi zake
ndiyo itakayosaidia kuhakikisha anakamilisha studio hiyo kwa muda.
EmoticonEmoticon