KAMA ilivyo kawaida yangu, jana Nilipata nafasi
ya Kupita katika Mtaa wangu wa BUGARIKA, jijini Mwanza.
Nashukuru mungu huwa nina Chama kubwa ambalo
huwa tunajumuika kupiga Story za hapa na pale hasa Muziki na masuala mengine,
Huku tukipata “UJI” wa jioni, ambao husukuma Story zetu.
Lakini wakati stoty Zimenoga, Walikuja ghafla
Vijana hawa wawili, AMANDOLA na TIZZO MIPANGO, ambao ninawafahamu vizuri maana
tunaishi pamoja Mtaa mmoja.
Katika kitu ambacho nilikinukuu kutoka kwa
AMANDOLA na TIZZO ni kwamba “HATUJAKATA TAMAA, LAKINI TUTAFANYAJE KAMA HUKO JUU
KUMEZIBWA?”
Wawili hawa wanazo nyimbo zaidi ya Mbili na wote
kwa pamoja wanafanya kazi vziuri sana, ingawa bado wanahitaji Support ya Dhati.
Niliwaza sana namna ya Kuwasaidia, nikasema
hapana, lazima hili nilifikishe TTM, ili tufanye kitu ambacho kinaweza
kueleweka kabisa..
Wanachokililia AAMANDOLA na TIZZO, ni Kitendo
cha nyimbo zao Kuchukuliwa, lakini Mwisho wa siku hata hazipitiwi na
waliozichukua kwa sababu tu, hawana Muonekano wa Kisanii (Mavazi, magari, Viatu
vya gharama, Kusuka Rasta au Mengineyo)
Tofauti na hapo, hata watu wanaoahidi
kuwasaidia, bado wanawakimbia na hata Kushindwa kupokea Simu zao, pale
wanapowapigia na Kuwakumbusha kile Walichopanga.
Lakini Ngoja Nifanye kitu kimoja, Sikiliza Hii
Track yao, inaitwa DEEJAY
EmoticonEmoticon