HUWA ni mara Chache sana Kusikia Tukio kama Hili hasa kwa Celebrities
wakubwa, licha ya Kwamba ni mara Nyingi Celebrities huwa Wanakwaruzana na
watoto wao.
Kiukweli hatuwezi kusema kuwa Ni Story ya Kufurahisha ambayo imetua
Kunako Meza ya TEAM TUKO MBELE.
RAPPER Young Jeezy ambaye alitambulika sana Kupitia Kwaju Zito la BLACK
PRESIDENT, hivi sasa anashikiliwa na Polisi Nchini marekani na huenda
akafunguliwa mashtaka ya Kujeruhi pamoja na Kutishia Kumuua Mtoto Wake
Kwa Mujibu wa taarifa Kutoka Mamlaka Husika, Tukio hilo lilitokea Mnamo
Mwaka 2012, na hatimaye kukamatwa Siku ya Ijumaa iliyopita.
MTONYO WENYEWE UKO
HIVI.
Inasemekana Kuwa JEEZY alimpa kipigo Mtoto wake huyo wa Kiume, huku
akimrusha kutoka Bafuni na Kupitia katika Mlango wa Kioo, jambo lilimfanya
Kijana huyo Kuanguka kwa Kupiga Kichwa Chake Chini.
Aidha TTM (TEAM TUKO MBELE) Imeendelea Kutonywa Kuwa, JEEZY
Hakuishia hapo, bali alimfuata Mtoto wake huyo na Kuanza kumchapa Ngumi Pale
Pale chini alipokuwa ameanguka, kasha akamburuza Mpaka Chumbani kwa na Kuanza
kumpa makonde ya Kutosha huko Huko Chumbani.
Pia imefahamika Kuwa, JEEZY alitamka maneno Ya Kutishia Kumuua mtoto wake
Mara Kadhaa wakati akimpa Kifinyo hicho, na Hata kudiriki kumwambia atampasua
Kichwa chake Kwa Risasi.
Hata Hivyo JEEZY alionekana kukiri na Kuiheshimu Kibali cha Kukamatwa, na
alisalimisha Kiasi cha Dolar za Kimarekani 45,000 sawa na takribani Tsh MILIONI 67 na LAKI 5
Pia Jeezy aliua Story Kwa Kusema kuwa, anaamini Ishu Hiyo itakwisha
kabisa na kila Kitu Kitakuwa Byee baada ya Muda Kadhaa
EmoticonEmoticon