FREEWAY RICK ROSS ambaye Ndiye anayedaiwa kuwa mmiliki wa Jina la
RICK ROSS, ametoa Tamko kuhusu Rick Ross “Rozay” kuchukua Jina lake na hata
Kupata Ushindi mahakamani.
Akizungumza Kwa Uchungu kuhusu Hilo akiwa na Hisia kali, Freeway Rick Ross amesema kuwa binafsi yeye
kama yeye anauheshimu Muziki wa HIP HOP, na hata baadhi ya wasanii ni Marafiki
zake.
Pia Freeway ameongeza Kuwa, Kwa kuwa Muziki wa Hip Hop
Unazungumzia Ukweli, Huwezi kutoka hapa na Kwenda Kule ukajitapa Kuwa Unafanya
Muziki wa Hip Hop, na hip Hop Ipo katika damu yako wakati Bado unasema Uwongo
kwa jamii hasa Vijana
Free way amezidi kudai Kuwa, anastaajabishwa na Mmoja wa maofisa
wa Zamani (Rick Ross) kuamua Kutumia Jina lake na Kila Kitu chake ili aweze
kupata Umaarufu na hata eti kukubalika Kwa jamii kuwa Ni Mtu wa watu, na
hatimaye kupata mafanikio makubwa.
Kitu Hicho kimeonekana kumuudhi sana Free way Rick Ross huku akizidi kusisitiza
Kuwa, bado atazunguka kila eneo husika ikiwemo katika Shule mbali mbali, ili
aweze kutoa Elimu na Kuzungumza Ukweli kuhusu yeye, maisha yake na madawa ya
kulevya, pamoja na mambo ya Msingi ambayo kijana anatakiwa kuyafanya.
Pia Free way amemalizia kwa kusema kuwa, yuko Mbioni kuachia
kitabu chakekinachomuhusu yeye na maisha yake, pamoja na Filamu ambayo itakuwa
na mafunzo kwa vijana.
EmoticonEmoticon