Wanamgambo wa kundi la al Shabab wametangaza marufuku ya kutumiwa intaneti katika maeneo ya Somalia
yaliyo chini ya udhibiti wao.
Kundi hilo limetoa muda wa siku 15 kwa
mashirika yote yanayotoa huduma ya intaneti kusitisha huduma zao.
Taarifa iliyotolewa na kundi hilo
imeeleza kuwa, kampuni au mtu yeyote ambaye hataheshimu ONYO hilo atachukuliwa kuwa anashirikiana na adui. Hata hivyo waasi hao wa Somalia
hawakueleza ni kwa nini wamechukua uamuzi huo.
Kundi la as Shabab lenye misimamo
mikali na mtizamo finyu kuhusu dini ya Kiislamu, limefurushwa katika miji
mikubwa ya Somalia kwa ushirikiano wa vikosi vya nchi hiyo na askari wa kulinda
amani wa Afrika walioko Somalia (AMISOM).
Hata hivyo bado wanamgambo wa kundi
hilo wanadhibiti baadhi ya maeneo ya nchi hiyo.
EmoticonEmoticon