Polisi ya Nigeria imetangaza habari ya kuuliwa watu 10 huko
kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Polisi hiyo imetangaza kuwa, mauaji hayo
yalijiri hapo jana baada ya kundi moja la watu wenye silaha kukishambulia
kijiji cha Njilang katika mkoa wa Adamawa kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
Watu tisa wengine wamejeruhiwa katika shambulizi hilo.
Mashambulizi ya kijiji cha Njilang ni katika mfululizo wa mashambulizi
yanayoendelea dhidi ya maeneo ya mpakani kati ya Nigeria na Cameroon. Baada ya
watu wenye silaha kutekeleza shambulio hilo, walikimbilia nchini Cameroon.
Siku ya Ijumaa Martin
Nesirky Msemaji wa Umoja wa Mataifa alitangaza kuwa, watetezi wa haki za
binaadamu wana wasiwasi mkubwa kutokana na kuendelea kwa machafuko huko
kaskazini mashariki mwa Nigeria, machafuko ambayo yamekuwa yakisababisha mauaji
na majeraha kwa raia wa kawaida.
EmoticonEmoticon