ZANZIBAR,
Balozi Mdogo wa Jamhuri ya Watu wa China
Zanzibar Bibi Chen Qiiman akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali
Iddi. Mazungumzo hayo yalifanyika katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar iliyopo ndani ya Jengo la Baraza la Wawakilishi
Mbweni nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .
Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China
inatarajia kuikabidhi Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar jengo jipya la Skuli ya Msingi ya
Mwana kwerekwe C katika kipindi cha siku chache zijazo baada ya kukamilika
ujenzi wake.
Ujenzi huo umekuja kufuatia ziara ya aliyekuwa Naibu Waziri
Mkuu wa China Bw. Hui Liangyu ambae ameshastaafu aliyoifanya Zanzibar
na kutia saini Mkataba kati ya serikali yake na Zanzibar katika masuala ya Uchumi na Ufundi
ukiwemo pia mradi huo wa ujenzi wa skuli ya Mwanakwerekwe C.
Mkataba huo uliotiwa saini umelenga kuipatia Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar jumla ya RMB Milioni Sitini { 60,000,000 }
sawa na shilingi za Kitanzania Bilioni 14.8 ambapo kati ya fedha hizo ujenzi wa
skuli hiyo pekee umegharimu jumla ya dola za kimarekani Milioni 1.6.
Balozi Mdogo wa China
aliyepo Zanzibar Bibi Chen Qiiman alieleza hayo wakati akizungumza na Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar BaloziSeif Ali Iddi
hapo Katika Ofisi yake iliyopo katika Jengo la Baraza la Wawakilishi liliopo
Mbweni Nje kidogo ya Mji wa Zanzibar .
EmoticonEmoticon