MWILI wa marehemu rais Hugo Chavez wa Venezuela , umelazwa katika kituo cha mafunzo ya
jeshi katika mji mkuu Caracas
Mapema leo mwili wa marehemu Chavez ulipitishwa kwenye umati
mkubwa wa wafuasi wake katika mitaa ya mji mkuu Caracas .
Watu wengi waliangua kilio huku wakichukua picha za kiongozi
wao aliyefariki dunia .
Mama yake na watoto wake walikusanyika mbele ya jeneza kutoa
heshma zao .
Makamu wa rais Nicolas Maduro anaongoza shughuli hiyo.
Mwili wa rais Chavez umepelekwa katika chuo cha kitaifa cha
mafunzo ya kijeshi ambapo utazikwa kesho Ijumaa.
Bwana Chavez alifariki akiwa umri wa miaka 58 baada ya
kuugua Saratani kwa zaidi ya miaka miwili.
Maelfu ya watu awali walikwenda barabarani mjini Caracas kutoa heshima zao za mwisho kwa Chavez wakifuatana
na gari lililokuwa limebeba jeneza lake
kuelekea katika chuo cha
mafuzno ya jeshi.
Mazishi ya kitaifa ya Chavez yatafanyika Ijumaa.
Mkuu wa ulinzi wa Rais alinukuliwa akisema kuwa alikuwa na
bwana Chavez alipofariki.
Generali Jose Ornella, alisema kuwa Chavez alifariki
kutokana na mshtuko wa moyo na katika siku zake za mwisho kabla ya kifo cha
ealisema angependa kuendelea kuishi.
Jeneza lake
lililokuwa limefunikwa
bendera ya nchi hiyo uliwekwa katika ukumbi ambao ni kumbukumbu ya waliopigania
uhuru wa watu wa Amerika ya Kusini
Maelfu ya watu walipanga foleni kutoa heshima zao za mwisho
kwa marehemu Chavez, wakiwemo maafisa wa serikali na viongozi wa Amerika ya
Kusini,kama Rais wa Bolivia Evo Morales na Rais wa Argentina Cristina Fernandez
de Kirchner.
EmoticonEmoticon