Mi Sidhani kama tulikosea kumuita
Justin Bieber “The Majanga Boy”, sababu kila anachokifanya tunahisi na hata
kubaini kuwa ni majanga matupu.
Sasa Bwana Mdogo huyu amekuja na
Hili Lingine..
Justin Bieber, ambaye Hivi sasa ana
Umri wa Miaka 19, na anajihusisha na Muziki wa Pop, alitoa kauli Moja tu ya
Kuwa anastaafu Muziki wakati akigonga Interview na Kituo Cha Redio cha POWER
106 Kilichopo Nchini marekani, na hata Kuirudia Tena kauli hiyo wakati anafanya
Interview na Kituo cha TV cha E News.
Lakini Kwa Mujibu wa Msemaji wake,
Inaswemekana kuwa Sio Kweli, bwana Mdogo Bieber hatoacha Muziki, na Ni Kitu
ambacho hakiwezi kutokea.
Pia Mitonyo Imezidi Kuvuja kuwa,
huenda siku anatamka Hiyo kauli ya Kustaafu Muziki, alikuwa tayari ameshachoma
Mmea Korofi, yaani BANGI, hivyo inawezekana kabisa Ile haikuwa akili yake Muda
Ule.
Pia Mitonyo inadai Kuwa, Kabla
hajaingia katika Studio za POWER 106 RADIO, Gari la Justin Bieber lilionekana
likwasili hapo huku Likitoa Moshi Mkubwa kutoka ndani ya Gari, jambo ambalo
linawafanya waamini kuwa, Mkali huyo Mdogo wa Pop, alikuwa anachoma Mmea
Korofi.
Pia akiwa katika Studio Hizo, Bieber
alitoa Taarifa kwa Media mbali mbali ambazo humuandama mara kadhaa kuwa,
wamekuwa wakiamini yeye ni Mkorofi na Mwenye Kiburi, jambo ambalo anadai Si
Kweli, kwani anawapenda, na Kuwajali Mashabiki zake.
EmoticonEmoticon