Wakenya wamehimizwa kuzingatia maridhiano na kusameheana wakati taifa hili likijiandaa kuadhimisha miaka hamini tangu kupata uhuru.
Wito huo umetolewa na rais Uhuru Kenyatta.
Rais Kenyatta amesema kuwa licha ya changamoto kuu zinaoikabili nchi, Wakenya wanastahili kuwa pamoja na kutoruhusu changamoto za binafsi kuathiri maendeleo ya taifa.
Wakati huohuo, amerejea kauli aliyotoa kabla ya uchaguzi mkuu mwezi Machi, kwamba kesi inayomkabili ni suala lake binafsi huku akiwahimiza Wakenya kuendelea na maombi .
Amesema haya siku bili tu baada ya Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa kukataa ombi la Umoja wa Afrika kutaka kesi ya rais na naibu wake katika mahakama ya ICC ziahirishwe.
Baada ya kukataliwa kwa ombi hilo, macho ssa yanaelezwa kwa mkutano wa mataifa 122 wanachama wa mahakama ya ICC wiki hii.
Mkutano huo utaanza tarehe 20 hadi 28 mwezi Novemba, nchini Uholanzi.
Uingereza ambayo haikupiga kura katika Baraza la Usalama la Umoja wa mataifa Ijumaa iliyopita, imesema mkutano huo wa wiki hii utatoa fursa muafaka ya kujadili suala la Kenya.
Pia Nchi ya Uingereza , ambayo ni mwanachama wa kudumu katika baraza hilo, inapendekeza mabadiliko ili rais na naibu wake wasihudhurie kesi dhidi yao, ila tu zifanyike kupitia video.
EmoticonEmoticon