Baada ya Kutaka Kufungua mashtaka dhidi ya Adui yake
Frank Ocean walipozichapa kunako Studio moja Nchini marekani, Breezy ameamua
kuchukua Hatua nyingine kumshtaki Shabiki wake wa Kike..
Kama Utakuwa unakumbuka Vizuri, Breezy aliwahi
kufunguliwa Mashtaka na Shabiki yake mmoja wa Kike,kwa madai kuwa alimsukuma
katika UKUMBI wa HEAT ULTRA LOUNGE, alipokuwa akiondoka akiwa na watu wake wa
karibu.
Lakini baada ya uchunguzi wa kina Kufanyika,
ikabainika Mwanadada huyo anayefahamika kwa Jina la DEANNA GINES hakusukumwa na
Chris katika Eneo la V.I.P alipokuwa amekaa, ila yeye Mwenyewe ndiye alikuwa
Mkorofi.
Kwa mujibu wa Mmiliki wa CLUB hiyo, inasemekana
kuwa DEANNA mwenye umri wa Miaka 24, alijaribu kupanda Mahali ambako Breezy
alikuwa, lakini ilishindikana baada ya Kuzuiwa na Baunsaz waliokuwa
wakihakikisha Suala Zima la Ulinzi kwa Breezy Linapatikana.
Lakini baada ya bibie huyo kutolewa mahali hapo
na Walinzi hao, Inasemekana alivua “Michuchumio” na kuanza Kuwaponda, yaani
kuwarushia.
Kwa mujibu wa mashtaka yaliyofunguliwa awali na
Mrembo huyo, Chris Breezy alikuwa anatakiwa kumlipa Mwanadada huyo Dolar za Kimarekani 25,000
sawa na takribani Shilingi za Kitanzania 37,500,000.
Lakini kwa hivi sasa, Chris Brown ameamua
kufungua Kesi ya Kuzalilishwa na Mwanamke huyo, kwani hata hivyo anadai kuwa
hawakupata hata nafasi ya kukaribiana kutokana na Ulinzi uliokuwepo, na pia
alimuona akitembea Vizuri Usiku wote
ule, jambo ambalo lilimchanganya Breezy kuwa ni Mguu gani uliojeruhiwa
EmoticonEmoticon