Waziri Mkuu wa Uingereza David Cameron ameandaa mkutano wa
kimataifa jijini London utakaojadili njia za kuisaidia Somalia kumaliza zaidi
ya miongo miwili ya machafuko.
Mkutano huo utajikita zaidi katika masuala ya kujenga upya
vikosi vya ulinzi na kukabiliana na ubakaji ambalo ni suala linalooonekana kama
mwiko.
Somalia inatafsiriwa kama taifa lililoshindwa, lililokumbwa
na vuguvugu la wanamgambo wa Kiislamu, uharamia na ukame tangu mwaka 2010 hadi
2012.
Takriban watu saba waliuawa katika mlipuko wa bomu kwenye
gari uliotokea katika mji mkuu Mogadishu siku ya Jumapili. Kundi la Al – Shabab
ambalo lina mafungamano na Al – Qaeda linadai kuhusika na shambulio hilo.
Mkutano huo ambao utakua chini ya uenyekiti wa Bw. Cameron
na rais wa Somalia Hassan Sheikh Mahamoud unafuatia mkutano kama huo
uliofanyika London na jijini Istanbul nchini uturuki mwaka jana, huku wasiwasi
ukiongezeka katika jumuiya ya kimataifa kwamba Somalia imegeuka hifadhi ya
wanamgambo wenye mahusiano na al Qaeda.
“Ninamatumaini kwamba, wote tunaweza kuafikiana kuhusu
mpango wa usalama wa muda mrefu, ambao utamaliza vitisho vya Al Shabab moja kwa
moja,” alisema Bw. Cameron.
“Pia ninamatumaini tutaboresha uwazi na uwajibikaji ili watu
wafahamu wapi rasilimali zinakwenda. Pia tunahitaji kuendelea na mchakato wa
kulijenga taifa la Somalia, ikiwemo mikoa yote ya Somalia na nchi jirani hali
kadhalika.”
Mchambuzi wa masuala ya Somalia wa BBC, Mary Harper anasema,
kumekuwa na mabadiliko ya ghafla nchini humo katika kipindi cha mwaka mmoja
uliopita.
EmoticonEmoticon