UHURU Kenyatta ndiye Rais wa nne wa Jamuhuri ya Kenya baada ya tume ya uchaguzi kumtangaza
kushinda uchaguzi wa kihistoria wa Kenya .
Ni baada ya siku tano tangu wakenya kupiga kura kuwachagua
rais, magavana, maseneta , waakilishi wa bunge, waakislihi wanawake na
waakilishi wa wodi.
UHURU KENYATTA NA MKEWE |
Uhuru alipata zaidi ya asilimia hamsini ya kura
zilizohitajika ili kupata ushindi kulingana na mahitaji ya katiba mpya ya nchi.
Matokeo hayo yalionyesha kuwa Uhuru Kenyatta ameshinda na
hivyo kuepuka duru ya pili ya uchaguzi.
Takwimu kutoka tume ya uchaguzi zinasema Kenyatta ameshinda
asilimia hamsini nukta tatu za kura zote zilizopigwa.
Tume ya uchaguzi ilichukua zaidi ya masaa matano kukagua
hesabu ya kura hizo kabla ya kutangaza matokeo hii leo siku tano baada
yawakenya kupiga kura.
Matokeo yaliyotolewa na tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa
Uhuru alipata kura 6,173,433 huku mpinzani wake Raila Odinga akipata 5,340,546
Kenyatta anakabiliwa na mashtaka katika mahakama ya
kimataifa ya ICC kuhusiana na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka wa
2007.
Awali duru zilisema iwapo Kenyatta atakabidhiwa ushindi
katika raundi ya kwanza, mpinzani wake waziri Mkuu Raila Odinga atakwenda
mahakamani kupinga matokeo hayo.
Tume hiyo pia itatangaza mshindi wa uchaguzi huo na vile
vile kama mshindi huyo ametimiza masharti ya kikatiba ya kutangazwa kuwa rais
wa nne wa Kenya .
UHURU KENYATTA NA WILLIAM RUTO |
Kamishna Yusuf Nzibo alitoa taarifa hiyo kwa niaba ya
Mwenyekiti wa Tume Isaack Hassan.
Vile vile mgombea huyo pia lazima awe ameshinda asilimia 25%
katika nusu ya County zote 47 nchini kenya .
Awali Waziri Mkuu Raila Odinga alikuwa amewaalika waandishi
wa habari nyumbani kwake kwa mkutano maalum ili azungumzie maswala ya matokeo
ya urais lakini baadaye mkutano huo uliakhirishwa hadi siku ya Jumamosi , baada
ya tume ya uchaguzi kutoa tangazo lake la mwisho.
EmoticonEmoticon