Afisa Utawala wa Malawi Council For The Handicapped, Mrs. Clara Fatch kutoka Nchini Malawi, akinionesha Bidhaa zinazozalishwa na Watu Wenye Ulemavu Nchini Malawi, katika Maonesho ya Wanawake Wajasiriamali Yanayaofanyika katika Viwanja vya Mnazi Mmoja, Jijini Dar es Salaam Tanzania
Bidhaa Hizo ambazo zinazalishwa na Walemavu kutoka Nchini Malawi, katika Shirika la Malawi Council For The Handicapped, zikiwa zinapendeza.
Magauni, Madela, Na Tshirt pamoja na Vitambaa vya Kupamba Majumbani na Maofisini
Mrs. Fatch akionesha Mkoba Ulioandikwa "ALAWI AFRICA", uliotengenezwa na walemavu
Wateja wakipokea Maelezo Kutoka kwa Wakina mama kutoka Malawi, juu ya Bidhaa bora zinazozalishwa na Walemavu.
Mapambo Mazuri yakiwa Katika Maonesho
Mrs. Fatch akinifafanulia Jambo kuhusiana na Bidhaa Zote zilizotengenezwa na Walemavu, kutoka katika Shirika Hilo.
Na Frank M. Joachim, DSM
Walemavu Nchini Tanzania Bado wana fursa Madhubuti ya kufanya Makubwa katika kujitafutia Kipato chao ili kuboresha Maisha yao ya Kila siku ikiwa Ni Sehemu kubwa ya Maendeleo ya Binafsi, jamii inayowazunguka, na Taifa Kiujumla.
Hayo Yameainishwa Mapema leo hii, baada ya Kufanya Mazungumzo na Afisa Utawala wa Shirika la MALAWI COUNCIL FOR THE HANDICAPPED liliko Nchini Malawi, Bi. Clara Fatch (Pichani), katika maonesho ya wanawake wajasiriamali yanayoendelea katika Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Shirika hilo ambalo Makao yake Makuu ni Nchini Malawi, Linajishughulisha na Kusaidia walemavu wenye Uwezo na Kipaji binafsi katika kuzalisha Bidhaa Mbali mbali kwa Matumizi mbalimbali.
Aidha Bidhaa zote zilizooneshwa katika Picha hapo juu ni nguvu kubwa ya Walemavu, hali amabyo inatoa hamasa na fursa kwa Walemavu wa Kitanzania kutokukaa na kuamini kuwa Ulemavu wao ndio Mwisho wa Maisha yao.
"Disability is not inability"
EmoticonEmoticon