REPIN ROCK CITY

REPIN ROCK CITY

TUMA TRACK YAKO

JOHANNES KANANI, Kijana Mwenye HAZINA KUU 3, zianzoweza kuleta mabadiliko Katika TASNIA KUU MBILI.

2:43:00 AM

Johannes Kanani, akiwa katika Chumba cha Kurushia Matangazo, (Studio Broadcasting), ikiwa Ni moja Ya Sehemu ya Kipaji Chake.


Hiyo Ni Tshirt ya ROYAL COLLEGE OF TANZANIA (RCT), Chuo Ambacho Johannes Kanani anachukua Stashahada yake ya Uandishi wa Habari na Utangazaji (Diploma in Journalism) 


Na Frank M. Joachim

JICHO KWA JICHO.
Kwa mara ya kwanza ninamfahamu Kijana huyu, ilikuwa ni Mwaka 2011, akichukua Astashada ya Ya uandishi wa Habari na Utangazaji (Certificate in Journalism) Katika Chuo cha Royal, Kipindi hicho nikiwa kama Programme Manager katika Radio ya Chuo, Royal Fm, 104.6 MHz. Sikufahamu kama ni Mtu mwenye Hazina Kuu Tatu a,mbazo zilinifanya niweze kumuona ni Kiumbe wa ajabu sana, anayeweza kuitumia Vema Hazina moja baada ya Nyingine kwa Nyakati Husika.

Ukaribu wangu na yeye uliweza kunifanya nianze kufahamu utundu wake na kubaini kuwa Ni Silaha inayoweza Kuleta Mabadiliko Makubwa katika Tasnia ya Utangazaji na Soko la Muziki Duniani Kote.
Umakini wake katika Taaluma yake, umemfanya kuwa Mtukutu hasa wa kufahamu mambo Lukuki katika Ulimwengu wa Vipaji vingi.

NINAMCHOKONOA HIVI...
Kanani ni Kijana Mtanashati, Very Smart and Valuable  kiasi kwamba amejikita kuwa Kijana wa Pekee sana hasa Kisifa, si Katika Chuo chake tu, bali hata Katika Jamii ambayo inamzunguka Kwa Ujumla.
Rangi yake Nyeusi inayoshamiri katika Ngozi Yake Humfanya ajivunie Uafrika na Mvuto aliojaliwa na Mwenyezi Mungu, kwani anajiona na anaamini kuwa anabahati kubwa sana kuzaliwa Barani Afrika, hasa Nchini Tanzania.
Tabasamu lake lenye kila ishara ya kuonesha kuwa ni Mcheshi, Mkarimu na Mwenye Busara, huongeza hamasa kwa Kijana yeyote yule kutamani kufanya kazi yoyote ile pamoja na JOHANNES KANANI.
Kiujumla Kanani ni Mrefu wa Wastani, Makini sana, Mcheshi na hasa Mbunifu katika Masuala mbali mbali ya Taaluma yake.

HAZINA ZAKE KUU TATU ALIZOJALIWA
1. MTANGAZAJI (Radio & Tv Presenter) mwenye Kipaji, Lafudhi mwanana, Sauti yenye kuhamasisha Hadhira, na Lugha thabiti inayopendeza

2. MUIMBAJI na MTUNZI mzuri wa Nyimbo za Injili (Gospel Singer)

3.MZALISHAJI MUZIKI (Music Producer) mzuri, anayetumia ubanifu na Ufanisi Mzuri sana katika Kazi Yake, ili kukuza Soko la Muziki wa Injili.

RANGI ANAZOPENDELEA.
Johannes Kanani anapendelea Rangi ya aina yoyote ile, maana anamini kilicho kizuri, ni Kizuri tu, hata kikibaguliwa, kitabaki kuwa Kizuri.

FACEBOOK GROUPS ANAZOVUTIWA NAZO
1. Ndimu Swaggalists (Promo for Machini)
2. Royal College Of Tanzania (RCT)
3. May 2011-2012 Intake ROYAL COLLEGE OF TANZANIA people and their Friends.

CHAKULA ANACHOPENDELEA
Ugali Samaki.

KINYWAJI.
Maji Safi na Salama

Share this

Related Posts

Previous
Next Post »

MNADA BANNER